Posts

ijue sherua ya mirathi

SHERIA YA MIRATHI YA TANZANIA SHERIA YA USIMAMIZI WA MIRATHI SURA YA 352 YA SHERIA ZA TANZANIA 1. SHERIA HII INASHUGHULIKA NA MAMBO YAPI NA INA LENGO GANI HASA? Lengo kuu la sheria hii ni kutoa utaratibu wa kusimamia mali za marehemu baada ya kifo chake ikiwamo kuhamisha umiliki wa mali hizo kutoka kwa marehemu kwenda kwa watu wenye haki ya kuzipata mali hizo.Nia hasa ni kwamba mali alizoacha marehemu zisibaki zikiharibika na kupotea bure,au warithi halali au watu wenye maslahi na mali za marehemu,kwa mfano wale wanaomdai hawapotezi haki hiyo, bali awepo mtu ambaye atazisimamia na kuzigawa kwa wahusika wakiwamo wadai na kuepusha mgongano katika jamii husika.Hivyo sheria inamuweka msimamizi wa kugawa mirathi husika na mamlaka yake. 2. MAHAKAMA ZIPI ZINA MAMLAKA YA KUSIKILIZA MASUALA HAYA Mirathi inaweza kufunguliwa katika mahakama mbalimbali kutegemea na sheria itakayosimamia mirathi husika. v Kama sheria ya kimila itatumika katika kugawa mirathi basi shauri