Posts

Showing posts from September, 2017

Dhania ya mwanamke na mwanaume kuchukuliwa kama wanandoa baada ya kuishi pamoja kwa mda fulani

Image
Dhana ya kuchukulia ndoa Kuna dhana inayokanushika (rebuttable   presumption) kuwa mwanamme na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria   japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.   (i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamme wameishi pamoja kwa muda wa miaka miwili au zaidi kwa mfululizo.   (ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma  unaowazunguka unawachukulia na  kuwapa heshima kama mke na mume.  (iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao  walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume  wakati walipoanza kuishi pamoja kama  umri ulikubalika kisheria.   (iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa   inayoendelea.  
Image
Vipengele gani vya kuzingatia ili wanaotaka kufunga ndoa wakubaliwe kisheria kufunga ndoa  (a) Ni lazima muungano uwe wa hiari Mume na mke wawe wameamua kuishi pamoja kwa ridhaa yao wenyewe. Hii inamaanisha kusiwe na kulazimishwa, kuhadaiwa kwa aina yoyote kwani   muungano kama huo utakuwa batili kisheria.   Ni kosa la jinai kushiriki katika shughuli ya ndoa ambayo mmoja wapo au wote wamelazimishwa kufunga ndoa.   (b) Muungano uwe ni kati ya mwanamke na mwanamme Muungano wa watu wa jinsia moja hata kama ni wa hiari muungano huo hautambuliki kisheria.   Pia mtu huhesabika mwanamke au mwanamme kutokana na   sehemu za siri alizozaliwa nazo na siyo alizozipata baadaye. Jamii inachukulia kuwa ndoa ni njia pekee   ya kujipanua, upanukaji huku ni kwa kuzaa watoto.   Kwa hali hiyo ili kupata watoto ni lazima ndoa iwe kati ya mwanamme na mwanamke. (c) Muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa ku...

Baraza la usuhishi wa Migogoro ya Ardhi Na Nyumba

BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA  Mfumo mpya wa utatuzi wa mi- gogoro ya ardhi na nyumba. 1. Utangulizi Sheria ya Ardhi Na.4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 za mwaka 1999 zimetungwa ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kutekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.  Sheria hizi zinaainisha vyombo pekee vya kushughulikia migogoro ya ardhi na nyumba. Vyombo hivyo ambavyo ni Mahakama kwa mujibu wa sheria hizi ni:-  i. Baraza la Ardhi la kijiji – ( The Village Land Council ).  ii. Baraza la kata – ( The Ward Tribunal )  iii.Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya- ( The District Land and Housing Tribunal )  iv.Mahakama Kuu-Kitengo cha Ardhi- ( The High Court-Land Division ).  v. Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ( The Court of Appeal of Tanzania ) Mfumo huu wa utatuzi wa migogoro unaoanzia katika ngazi ya Kijiji unalenga kuchukua muda mfupi na kutumia taratibu rahisi na shirikishi zisizokuwa na gharama kubwa kwa watanzania.  2. Sheria Na.2 ya mwaka...