Dhania ya mwanamke na mwanaume kuchukuliwa kama wanandoa baada ya kuishi pamoja kwa mda fulani
Dhana ya kuchukulia ndoa
Kuna dhana inayokanushika (rebuttable presumption) kuwa mwanamme na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971
ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.
(i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamme wameishi pamoja kwa muda wa miaka miwili au zaidi kwa mfululizo.
(ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma unaowazunguka unawachukulia na kuwapa heshima kama mke na mume.
(iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume wakati walipoanza kuishi pamoja kama umri ulikubalika kisheria.
(iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa
inayoendelea.
hahahahahah dogo upo vizuri sana
ReplyDeleteAhsante kwa elimu hiyo, maana inasaidia jamii yetu
ReplyDelete