Makosa yahusuyo udhalilishaji na yafananayo na hayo

(a) Katika Kifungu cha 89 cha Sheria hiyo inatamkwa kwamba mtu yeyote anayetumia lugha ya kudhalilisha aidha kwa kutamka au kwa ishara dhidi ya mtu yeyote katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani, mtu huyo atakuwa ametenda kosa la jinai na atakapotiwa hatiani atatumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.

(b) Katika kifungu cha 135 Sheria hiyo inatamkwa kwamba mtu yeyote atakayemdhalilisha mtu yeyote kwa kumbughudhi aidha kwa kutumia maneno, sauti au ishara au kitu kitakachoashiria matusi na endapo atapatikana na hatia kwa kosa hilo atapewa adhabu ya kifungo cha muda wa miaka mitano au kulipa faini ya fedha kwa kiasi kisichozidi shilingi laki tatu au adhabu zote mbili kwa pamoja.

(c) Katika Kifungu cha 138 D inatamkwa kwamba ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kufanya udhalilishaji wa kijinsia kwa mtu mwingine. Mtu yeyote mwenye dhamira ya kutenda uovu endapo atamshambulia mtu yeyote aidha kwa maneno au vitendo kwa nia ya kumuudhi au kumdhalilisha kujinsia mtu huyo atakuwa ametenda kosa na endapo atatiwa hatiani atapewa adhabu ya kifungo cha miaka mitano au kulipa faini ya shilingi laki mbili au kupewa adhabu zote mbili.

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)