Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009
Maana ya Mtoto
Kwa mujibu wa Sheria ya mtoto ya mwaka 2009(The Law of Child Act) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989(Convention On the Rights of Child), mtoto ni kila banadamu aliye chini ya umri wa miaka 18 kulingana na kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Mtoto Ya mwaka 2009
Sababu za kuwa na ulinzi wa haki za mtoto ni pamoja na;
➣ Watoto ni binadamu, wana haki sawa;
➣ Watoto hawana sauti ya kujisemea au hawana uwezo wa kupigania haki zao wenyewe;
➣ Kuwepo kwa wimbi kubwa la ukiukwaji wa haki za watoto mfano ukatili dhidi ya mtoto, utesaji na ubakaji
Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 inashughulikia haki za watoto Tanzania. Sheria hii inajumuisha mambo mbalimbali ya kukuza, kulinda, na kuhifadhi ustawi wa mtoto; masharti ya unajibishaji wa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa; masuala ya kulea, kuasili na uangalizi. Pia inatoa maelekezo na masharti yanayohusu mtoto anapokuwa katika mgogoro na sheria.
Sheria hii inatumika kutetea masuala yote ya kuboresha, kulinda na kuhifadhi ustawi wa mtoto pamoja na haki zake.
Kwa mujibu wa sheria hii mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane. Sheria hii inafanunua zaidi kuwa mtoto ni pamoja na mtoto yatima, mtoto aliye katika mazingira magumu, mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa, mtoto wa kuasiliwa, na mtoto anayelelewa katika vituo vya kulelea watoto.
Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009
➣ Haki ya kuishi (kifungu cha 9)
➣ Haki ya kupumzika
➣ Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa (kifungu cha 9(3)(a)
➣ Haki ya kutokubaguliwa(kifungu cha 5)
➣ Haki ya jina na utaifa (kifungu cha 6)
➣ Haki ya kuishi na wazazi wake (kifungu cha 7)
➣ Haki ya kupata huduma bora za elimu, malazi matibabu kwa ajili ya ustawi wake
➣ Haki ya kushiriki michezo na shughuli za kiutamaduni kifungu cha 9(2)
➣ Haki ya huduma za pekee kwa walemavu
➣ Haki ya kunufaika na kutumia kwa uangalifu mali za wazazi wake(kifungu cha 10)
➣ Haki ya kutoa maoni, mawazo kusikilizwa na kutoa maamuzi ya ustawi wake(kifungu cha 11)
➣ Haki ya kutoajiriwa katika ajira zenye madhara(kifungu cha 12)
➣ Haki ya kulindwa dhidi kudhalilishwa kijinsia.
Wajibu wa Jumla wa Mtoto Pamoja na haki za mtoto pia anawajibika katika maeneo yafuatayo;-
➣ Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamo wa familia; kifungu cha 15(a)
➣ Kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake wote na atawasaidia pale inapohitajika; kifungu cha 15(b)
➣ Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kimwili na kiakili kadiri ya umri na uwezo wake;
➣ Kutunza na kuimarisha mshikamo wa jamii na taifa; kifungu cha 15(d)
➣ Kutunza kuimarisha mambo mema ya utamaduni wa jamii na taifa kwa ujumla katika uhusiano na wanajamii au taifa.kifungu cha 15(e)
➣ Mtoto yeyote aliyepata mafunzo ya ufundi anawajibu wa kufuatilia kwa makini na kukubali kwa uaminifu, mafunzo aliyopewa na Mwalimu kwa kuhudhuria mafunzo na kuzuia uharibifu wowote wa makusudi na kutoharibu mali za mtoa mafunzo.kifungu cha 15(c)
Comments
Post a Comment