KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

KOSA LA KUGHUSHI VYARAKA MBALIMBALI
Kanuni ya Adhabu kifungu cha 333 kinaeleza nini maana ya kughushi ikiwa ni ni kutengeneza nyaraka ya uwongo kwa nia ya kudanganya au kuhadaa.
Kanuni ya Adhabu kifungu cha 335 kinaeleza kuwa. Mtu yeyote anayetengeneza nyaraka ya uwongo ambaye– 
(a) anafanya nyaraka ambayo ni ya uwongo au ambayo ana sababu ya kuamini kuwa si ya kweli; 
(b) anabadili nyaraka bila ya mamlaka kwa namna ambayo iwapo kubadili huko kungekuwa na mamlaka kungebadili matokeo ya nyaraka hiyo; 
(c) anaingiza katika nyaraka hiyo bila ya mamlaka , wakati nyaraka hiyo inaandikwa, jambo ambalo kama lingeruhusiwa lingebadilisha matokeo ya nyaraka hiyo; 
(d) anatia sahihi nyaraka – 
  • (i) kwa jina la mtu yeyote bila ya ruhusa ya mtu huyo, liwe jina hilo ni la yule anayetia sahihi hiyo au silo; 
  • (ii) kwa jina la mtu yeyote wa kubuniwa ambaye anadhaniwa kwamba yupo, iwe mtu wa kubuniwa huyo anadhaniwa kwamba ni wa jina sawa na aliyetia sahihi hiyo au sivyo; 
  • (iii) kwa jina linalofanywa liwe jina la asiyekuwa yule mwenyewe kutia sahihi nyaraka hiyo, na ambalo linakusudiwa likosewe kwa jina la huyo anayetia sahihi; 
  • (iv) kwa jina la mtu ambaye mwenye kutia sahihi nyaraka hiyo anajifanya ni yeye isipokuwa kwamba matokeo ya nyaraka hiyo inategemea utambulisho kati ya mtu anayetia sahihi na mtu aliyekubali ni yeye. 
Kanuni ya Adhabu kifungu cha 336. Nia ya kudanganya inadhaniwa kuwepo iwapo inaonekana kwamba wakati ambao nyaraka ya uwongo inatengenezwa kulikuwepo na mtu mahasusi anayejulikana au asiyejulikana ambaye anaweza kudanganywa, na kudhaniwa huko hakutakanushwa kwa uthibitisho kwamba mkosaji huyo alichukuwa au alikusudia kuchukua hatua za kuzuia mtu huyo asidanganywe, wala kwa kuwa alikuwa na haki au alidhani kwamba alikuwa na haki ya hicho kitu ambacho kitapatikana kwa nyaraka hiyo ya uwongo.
 ADHABU YA KUGHUSHI NYARAKA
kulingana na kanuni ya Adhabu, adhabu yake ni kifungo cha miaka 7

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)