Haki za Raia anapokuwa amekamatwa na polisi
Raia una haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako. 1.Mwulize jina lake 2.Mwulize namba yake ya uaskari 3.Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa. 4.Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa. 5.Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa. 6.Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika. 7.Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu. 8.Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakat...