Haki za Raia anapokuwa amekamatwa na polisi


Raia una haki ya kumwomba  askari ajitambulishe kwako.

1.Mwulize jina lake
2.Mwulize namba yake ya uaskari
3.Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
4.Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu,jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama
amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
5.Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia
rushwa.
6.Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapokituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa,
isipokuwa maelezo utakayoandika.
7.Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema
linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, naasiburuzwe kuandika tu.
8.Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
9.Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
10.Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
11.Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
12.Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa
na kufikishwa kituo cha polisi.

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)