MAKOSA YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE
MAKOSA YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE Makosa ya uzembe mbali ya kuwa makosa ya madai ambayo yaadhibiwa na sheria pia ni makosa ya jinai kulingana na sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 233. Mtu yeyote ambaye kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine yeyote:- (a) anaendesha gari lolote , baiskeli au piki piki katika barabara yoyote ya umma; au (b) anaendesha au kushiriki katika kuendesha au kufanya kazi katika meli yoyote; au (c) anafanya kitendo chochote kwa kutumia moto au kitu chochote kiwezacho kuwaka au kuacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambao inaweza kutokea kutokana na moto wowote au kitu chochote anachomiliki ambacho kinaweza kuwaka; (d) anaacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambayo inaweza kutokea kutokana na mnyama yoyote anayemmiliki; au (e) anatoa matibabu ya dawa au ya upasuaji kwa mtu yeyote ambaye amediriki kumtibu; au (f) anachanganya, a...