JE MKE ANAWEZA KUMUIBIA MUME WAKE, AU MUME ANAWEZA KUMUIBIA AU KUIBA MALI YA MKE.
Ni swali linaloulizwa na watu wengi sana wakitaka kufahamu kama mume na mke wanaweza kuibiana, kulingana na sheria yetu Kanuni Ya Adhabu (Penal Code)
Kifungu cha 264 Ili kuondoa mashaka, inatangazwa hapa kuwa mume anaweza kuwa na hatia kwa kumuibia mke wake au mke kwa kumuibia mumewe.
Hii inatokana na maana ya kisheria inayotolewa katika Kifungu cha 258 ya Kanuni Ya Adhabu, (1) Mtu ambaye kwa udanganyifu na bila ya dai la haki anachukua kitu chochote ambacho kina uwezo wa kuibwa, au kwa udanganyifu anabadili matumizi ya mtu yeyote tofauti na mmiliki wa jumla au maalum wa kitu chochote chenye uwezo wa kuibiwa, atakuwa anaiba kitu hicho.
(2) Mtu yeyote ambaye anachukua au anabadilisha kitu chochote ambacho kina uwezo wa kuibwa, anachukuliwa kufanya hivyo kwa udanganyifu iwapo anafanya hivyo akiwa na nia yoyote kati ya hizi, hii ni kusema-
ü  (a)nia ya la kumnyang’anya kabisa mmiliki wa jumla au maalum wa kitu hicho;
ü  (b) nia ya kutumia kitu hicho kama rehani au dhamana;
ü  (c) nia ya kukichukuwa kitu hicho kiasi kwamba wakati wa kukirudisha, ambapo mtu aliyekichukua au kukibadilisha anaweza kushindwa kutekeleza;

ü  (d) nia ya kukitumia kwa namna ambayo hakiwezi kurejeshwa katika hali kilivyokuwa wakati wa kukichukuwa au kukibadili

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)