MAKOSA YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE
MAKOSA
YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE
Makosa
ya uzembe mbali ya kuwa makosa ya madai ambayo yaadhibiwa na sheria pia ni
makosa ya jinai kulingana na sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu
Kifungu
cha 233. Mtu yeyote ambaye kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa
kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine
yeyote:-
(a)
anaendesha gari lolote , baiskeli au piki piki katika barabara yoyote ya umma;
au
(b)
anaendesha au kushiriki katika kuendesha au kufanya kazi katika meli yoyote; au
(c)
anafanya kitendo chochote kwa kutumia moto au kitu chochote kiwezacho kuwaka au
kuacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambao inaweza kutokea
kutokana na moto wowote au kitu chochote anachomiliki ambacho kinaweza kuwaka;
(d)
anaacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambayo inaweza kutokea
kutokana na mnyama yoyote anayemmiliki; au
(e)
anatoa matibabu ya dawa au ya upasuaji kwa mtu yeyote ambaye amediriki kumtibu;
au
(f)
anachanganya, anasambaza, anauza anasimamia au anatoa dawa yoyote au sumu au
kitu cha hatari; au
(g)
anatenda kitendo chochote, au anaacha kuchukuwa tahadhari ya kutosha dhidi ya
hatari yoyote kutokana na mashine yoyote ambayo iko chini yake au sehemu ya
mashine hiyo iko chini ya uangalizi wake ; au
(h) anatenda kitendo chochote, au anaacha
kuchukuwa tahadhari ya kutosha dhidi ya hatari yoyote inayoweza kutokea
kutokana na kitu chochote cha mlipuko kilichoko chini yake, atakuwa anatenda
kosa.
Comments
Post a Comment