MAKOSA YA JINAI YA UVIVU NA UZEMBE
MAKOSA YA JINAI YA
UZEMBE NA UVIVU
Sheria yetu ya kanuni
ya adhabu inatambua makosa ya uvivu na uzembe kama makosa ya jinai
yanayoadhibiwa kisheria, fungu la 176 ya kanuni ya Adhabu.
ü Kucheza
kamari kuwa ni kosa la jinai
ü Kufanya
umalaya
ü Kufanya
kitendo cha aibu mbele ya hadhara/ kufanya mapenzi mbele ya watu.
ü mtu
aliyeajiriwa chini ya ajira halali inayotambulika ambaye, bila udhuru halali,
anapatikana akichezacheza au kufanya mzaha wakati wa muda wa kazi, atahesabiwa
kuwa ni mtu mvivu na mzembe na atapaswa kulipwa faini isiyozidi shilingi mia
tano au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
ü mtu
anayetangatanga au anayejiweka katika mahali popote pa hadhara kwa kuomba au
kukusanya sadaka, kumtuma au kumhimiza mtoto kufanya hivyo;
ü mtu
anayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa
namna yoyote kwa njia ya kujisingizia au hadaa;
ü mtu
anakayeonekana ndani au kwenye au karibu na nyumba yoyote au katika njia au
barabara yoyote au mahali popote karibu na njia au barabara, au katika mahali
popote pa hadhara katika wakati na hali ambayo yapelekea kana kwamba mtu huyo
yupo hapo kwa jambo lisilo halali au la kikorofi;
atahesabiwa
kuwa ni mtu mvivu na mzembe na atapaswa kifungo kisichozidi miezi mitatu au
faini
Comments
Post a Comment