Maana ya dhamana kisheria




Dhamana(Bail)


Dhamana uhuru wenye masharti apewao mtuhumiwa au mshitakiwa wakati shauri lake likiendelea kupelelezwa, likiendelea kusikilizwa mahakamani au likisubiri matokeo ya rufaa yake. 


Misingi ya Dhamana Katiba ya nchi yetu inaeleza wazi kuwa kila mtu anastahili kuwa huru kwani binadamu wote wamezaliwa huru na wote ni sawa. 

Katika nchi inayoongozwa na kuheshimu utawala wa sheria kuna ile dhana ya kuamini kwamba kila mtu ni hana kosa hadi hapo atakapothibitishwa na mahakama kuwa ni mhalifu.(pressumption of innocence) 

Hii hali ya kuonekana kutokuwa na makosa mbele ya sheria inaleta msingi mwingine wa haki za asili za kimsingi ambazo zinasema mtu asihukumiwe bila ya kusikilizwa. 


Vile vile kila mtu anastahili kutambuliwa na kuheshimiwa utu wake. Kwa kutambua kanuni hizi za msingi Katiba imeendelea kusisitiza yakuwa ili kuhakikisha watu wote wako sawa mbele ya 4 Dhamana sheria, mamlaka ya serikali inapaswa kuweka taratibu nzuri na ambazo zitazingatia kuwa mtu yeyote anayeshtakiwa kwa kosa la jinai hapaswi kufanyiwa kama vile ameshatiwa hatiani kwa kosa aliloshtakiwa. 


KUMBUKA: Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba inasema kuwa: Ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo. Maelezo haya ya Katiba yana maana kwamba, mshitakiwa anatendewa kama mtu asiye na hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha kosa lake. Ili kukazia msimamo huu, sheria inatoa msingi kuwa mtu asiadhibiwe kabla hayapewa haki ya kusikilizwa utetezi wake. Kwa hali hiyo, kuwepo kwa utoaji wa dhamana kwa mshitakiwa ni kuendelea kuheshimu haki yake ya kuwa huru hadi atiwe hatiani kwa kosa analoshitakiwa. 


Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai imefafanua taratibu zote za utoaji wa dhamana na masharti yake.






Dhamana ni Haki(constitutional right) na Siyo Upendeleo Kwa kuwa dhamana ni haki ya mtu, hivyo anapoomba hapaswi kukataliwa bila sababu za msingi. Mahakamani na wanaharakati wa haki za Dhamana 5 binadamu wamesisitiza mara nyingi kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa pale anapotimiza masharti yake; kumnyima bila sababu ni kumkosesha haki ya msingi ya kuwa huru kwa mujibu wa sheria. Vile vile polisi au mahakama inapokataa kutoa dhamana ni lazima kuwe na sababu nzito zenye kuridhisha kabla ya kufikia uamuzi huo. 


Hapa Tanzania uzoefu umeonyesha kuwa ni kesi za mauaji, wizi wa kutumia silaha na uhaini tu ambazo kutokana na uzito wake mtuhumiwa hawezi kuwekewa dhamana ila kesi nyingine zote zilizobaki, mshitakiwa anayohaki ya kuwekewa dhamana, pindi akitimiza masharti ya dhamana na mahakama ikaridhika. hii kulingana na Kifungu 148(5) cha Sheria Ya Mwenendo Wa Makosa Ya Jinai


Kwa msingi huu dhamana ni haki ya mshitakiwa na kupewa dhamana ni katika kutimiza haki hiyo ya msingi. Mahakama inaweza kukataa kutoa dhamana iwapo itakuwa imeridhika kuwa kutolewa kwa dhamana kutaharibu maana nzima ya kesi hiyo kuwepo mahakamani, kutavuruga kesi hiyo, au mshitakiwa anaweza kupata madhara ikiwa ataruhusiwa kurudi kwa jamii. Hali hii ndiyo inayosababisha kesi za mauaji na uhaini kukataliwa dhamana kwani adhabu yake ni nzito (kifo) ambapo ni rahisi mshitakiwa kushawishika kutoroka.






MAMLAKA NA MAUDHUI YA DHAMANA 


Vyombo Vyenye Mamlaka ya Kutoa Dhamana Kutoa dhamana ni wajibu wa kisheria ambao unapaswa kufanywa kwa kuzingatia misingi na kanuni za sheria kwa hali hiyo siyo kila mamlaka inaweza kutoa dhamana. 


Dhamana ya Polisi (police bail)


Kwa ujumla kuna dhamana zitolewazo na Polisi na kuna zile zitolewazo na mahakama. Dhamana ya polisi hutolewa kwa mtuhumiwa aliyeko chini ya ulinzi na mkuu wa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa anashikiliwa. 

Kwa ujumla Polisi wanapaswa kumwachia mtuhumiwa baada ya kujidhamini mwenyewe kwa maandisi au kudhaminiwa na wadhamini wanaoaminika ikiwa: mtuhumiwa alikamatwa pasipo hati ya kumkamata mshitakiwa; au ikiwa baada ya upelelezi imebainika kuwa hakuna ushahidi wa kutosha; au ikiwa mashitaka yake siyo ya makosa makubwa; au ikionekana kuwa upelelezi wa ziada unahitajika na kwamba hauwezi kukamilika ndani ya saa ishirini na nne tangu kukamatwa mtuhumiwa. 

Muhimu: Ikiwa mshitakiwa ni mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na tano lazima aachiliwe mara Dhamana 7 mzazi au mlezi au ndugu au mtu yeyote mwenye kuaminika atakapomuwekea dhamana; Ni marufuku kwa afisa wa polisi kupokea fedha kama ada ya dhamana, au malipo yoyote kwa ajili ya kuendesha kesi, kutoa ushahidi, au kumkamata mtuhumiwa; 

Mtuhumiwa ana haki ya kupewa taarifa kamili kuhusu sababu za kukamatwa kwake, na haki ya kupata dhamana kwa mujibu wa sheria, na ikiwa Polisi atakataa kutoa dhamana kwa mtuhumiwa, ni lazima Polisi huyo abainishe kwa maandishi sababu za kukataa kwake. 


Dhamana ya Mahakama(court bail)


Dhamana ya Mahakama ni dhamana inayotolewa na mahakama baada ya mshitakiwa kusomewa mashitaka yake na kukana kosa. 

Kisheria dhamana hii ina lengo la kumruhusu mtuhumiwa kuwa nje ya mahabusu hadi pale mahakama itakapotoa hukumu. 


Dhamana hii huweza kutolewa na Jaji au Hakimu. Mahakama Kuu ya Tanzania ndiyo iliyo na uwezo wa mwisho wa kuamua kutoa dhamana au kutokutoa kwa yale makosa ambayo sheria inaruhusu dhamana. 


Kwa hali hiyo madhumuni ya dhamana ni kwamba hata kama mtu ameshitakiwa kwa kosa la jinai bado ana haki zake zote za kimsingi kwani bado 


Dhamana hajathibitika kisheria kutenda kosa hilo. Kwa kusema kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa ina maana kuwa pale mshitakiwa anaposhitakiwa anayo haki ya kuwekewa dhamana ila kuna mazingira yanayoweza kusababisha mshitakiwa asipewe dhamana.

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)