Uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kila mmoja haijalishi ni shehe, mchungaji au askofu



UHURU WA KUTOA MAONI


Ni haki ya kikatiba kabisa inatambuliwa kisheria


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Ibala ya


18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.


Hapa sheria imesema kila mtu haijalishi ni askofu, mchungaji au shehe ana haki ya kikatiba ya kutoa maoni yake


Pia Ibala 21(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.

Kanuni Ya Adhabu kifungu namba 63B(1)


Mtu hatakuwa ametenda kosa la uchochezi kama atatoa maoni


(a) kuonyesha kwamba Serikali imeongozwa vibaya au imekosea katika mwendo wake; au


(b) kutaja makosa au upungufu katika Serikali au siasa ya Serikali au Katiba ya Tanganyika kama ilivyowekwa na sheria, au sheria yoyote au katika usimamaji wa haki kwa kusudi la kutaka kuondosha au kusahihisha upungufu au makosa hayo; au


(c) kushawishi wakati wowote wa Tanganyika wajaribu kuleta mageuzo ya jambo lolote katika Tanganyika kwa njia ya halali; au


(d) kutaja kwa nia ya kuyaondosha mambo yoyote ambayo yameleta au yanaelekea kuleta chuki kati ya wakazi wowote wa Tanganyika au hisi ya chuki au uadui kati ya mbari au jamii ya watu mbali mbali wa Tanganyika

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)