Fidia kwa ardhi iliyotwaliwa kwa manufaa ya umma kulingana Sheria za Ardhi
FIDIA YA ARDHI NI NINI. Fidia ya ardhi ni stahili ambayo mwenye ardhi mmiliki anatakiwa kupata pale ambapo ardhi yake inatwaliwa/inachukuliwa na serikali kwa matumizi maalum ya serikali/umma. JE UNAWEZA KUIKATALIA SERIKALI ARDHI YAKO ISICHUKULIWE ? . Serikali inapotaka kumhamisha mwananchi na kuchukua ardhi yake kupisha mradi wa umma kisheria mwananchi hana uwezo wa kukataa. Hii ni kwasababu ardhi yote ni mali ya umma ambayo mdhamini wake mkuu ni serikali kupitia mamlaka ya rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa ardhi ni mali ya umma inayodhaminiwa na serikali/rais. Kwa hiyo mwananchi hawezi kuikatalia serikali kuchukua mali hiyo isipokuwa kisheria ni kuwa anayehamishwa apewe fidia. Hata ukiamua kwenda mahakamani kupinga kutwaliwa ardhi hautapinga kuwa serikali isichukue ardhi yako kabisa, isipokuwa utapinga kuhusu fidia, labda fidia ndogo au utaratibu mbovu uliotumika ku...