FAHAMU MISINGI YA SHERIA YA ARDHI YA TANZANIA



FAHAMU MISNGI YA SHERIA YA ARDHI YA TANZANIA

Ifuatayo ni misingi halisi ya ardhi kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo wa ardhi wa kitaifa (sera) na kutafsiriwa na sheria mbalimbali za nchi:

i. Ardhi yote ni mali ya umma na imekabidhiwa kwaRaisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya watanzania wote;

ii. Kulinda haki zote za miliki za ardhi zilizopo, yaani miliki ya ardhi ya kimila na ile ya kiserikali;

iii. Kugawa ardhi kwa haki na kwa raia wote wa Tanzania;

iv. Kudhibiti kiasi ambacho mtu mmoja au taasisi yaweza kumiliki na kutumia kwa mahitaji yake bila kuwaathiri Watanzania au wanajamii wengine;

v. Kuwezesha utumiaji endelevu wa ardhi katika shughuli za kiuzalishaji kwa manufaa ya wote;

vi. Kuhakikisha kwamba maslahi yeyote katika ardhi yana thamani na yanalindwa katika muda wowote wakati wa mapatano yanayoweza kuathiri thamani ya mmiliki;

vii. Kulipa fidia kamili na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki ya ardhi yake inafutwa, inabadilishwa au inaingiliwa kwa namna yeyote na serikali kwa manufaa ya umma na yeye kuathirika na zoezi hilo;

viii. Kuweka mfumo thabiti, wa wazi na rahisi katika kusimamia ardhi;

ix. Kuwawezesha raia wote kushiriki katika kutoa maamuziya mambo yanayohusiana na miliki na matumizi yako ya ardhi;

x. Kuwezesha uendeshaji wa bora wa soko la ardhi;

xi. Kulinda haki za wakulima na wafugaji wadogo vijijini na mijini kwa kudhibiti matumizi ya ardhi;

xii. Kuweka kanuni za sheria za ardhi ambazo zinapatikana kwa urahisi na zinazoeleweka kwa raia wote;

xiii. Kuwezesha kuwepo kwa mfumo huru, rahisi na unaofanya kazi kwa haraka katika suala zima la utatuzi wa migogoro ya ardhi;

xiv. Kutoa haki sawa kwa jinsia zote (mwanamke na mwanaume) kumilki, kutumia na kufanya shughuli yeyote kwenye ardhi bila kuweka mipaka yeyote; na

xv. Kuhimiza usambazaji wa taarifa zozote zinazohusu ardhi kwa raia wote wa Tanzania.

Kutwaa Njia hii hutumika pale ambapo mtu huingia katika eneo kama vile pori na kusafisha kisha kuliweka katika matumizi.

Njia hii ni kongwe sana hapa nchini. Pori linalosafishwa linaweza kuwa ardhi ya kijiji, hifadhi au ya jumla. Ni ngumu kutumia njia hii nyakati hizi, lakini bado inatumika katika

maeneo mengi ya Tanzania. Pale ambapo utatakiwa kufuata taratibu kama vile kusajili utatakiwa kutii amri hiyo. Kama utatakiwa kuhama eneo hilo basi mamlaka husika itatakiwa kulipa fidia ya maendelezo uliyoyafanya katika ardhi hiyo.

Hali kadhalika, mtu anaweza kutwaa ardhi kwa kuachwa akae kwenye ardhi au nyumba ya mtu fulani kwa kipindi kirefu kisichopungua miaka kumi na mbili (12) kama vile
yuko kwenye ardhi yake na kuweza kufanya kila atakavyo bila kukumbushwa, kukemewa, kulipishwa kodi au bila ya bughudha ya aina yeyote ya umiliki huhesabiwa kuwa

anamiliki ardhi ile kihalali. Hata hivyo, njia hii ya utwaaji haiwezi kutumika dhidi ya ardhi inayomilikiwa na taasisiya serikali. 

Kubadilisha Matumizi ya Ardhi kwa Manufaa ya Umma Ardhi inaweza kutwaliwa na matumizi yake ya awali yakabadilishwa kwa ajili ya uendelezaji wa matumizi mengine

kwa manufaa ya umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Utwaaji wa Ardhi ya Mwaka 1967, ardhi ya mtu binafsi au taasisi itatwaliwa kwa manufaa ya umma, mwenye ardhi anastahili kulipwa fidia
pindi azimio la utwaaji wa ardhi linapopitishwa.
Ibala ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoka inaeleza haki ya fidia kama haki ya msingi pale mali yako inapotwaliwa, lakini sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 inaeleza kuwa fidia ya ardhi inabidi itolewe kulingana na thamani ya Ardhi yenyewe na fidia yake iwe ya haraka bila kucheleweshwa( compensation to be fair, prompt and adquate

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)