Maana ya dhamana kisheria
Dhamana(Bail) Dhamana uhuru wenye masharti apewao mtuhumiwa au mshitakiwa wakati shauri lake likiendelea kupelelezwa, likiendelea kusikilizwa mahakamani au likisubiri matokeo ya rufaa yake. Misingi ya Dhamana Katiba ya nchi yetu inaeleza wazi kuwa kila mtu anastahili kuwa huru kwani binadamu wote wamezaliwa huru na wote ni sawa. Katika nchi inayoongozwa na kuheshimu utawala wa sheria kuna ile dhana ya kuamini kwamba kila mtu ni hana kosa hadi hapo atakapothibitishwa na mahakama kuwa ni mhalifu.(pressumption of innocence) Hii hali ya kuonekana kutokuwa na makosa mbele ya sheria inaleta msingi mwingine wa haki za asili za kimsingi ambazo zinasema mtu asihukumiwe bila ya kusikilizwa. Vile vile kila mtu anastahili kutambuliwa na kuheshimiwa utu wake. Kwa kutambua kanuni hizi za msingi Katiba imeendelea kusisitiza yakuwa ili kuhakikisha watu wote wako sawa mbele ya 4 Dhamana sheria, mamlaka ya serikali inapaswa kuweka taratibu nzuri na ambazo zitazingat