Haki Ya Uzazi Kwa MfanyaKazi Aliyeajiriwa

Uzazi na kazi sawa na sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini
Likizo ya Uzazi Mfanyakazi atalazimika kutoa notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu. Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi- 
(a) muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua; 
(b) katika tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa. 
Mfanyakazi hatatakiwa kufanya kazi ndani ya wiki sita baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake, labda tabibu awe amethibitisha kuwa anaweza kufanya hivyo.
Mfanyakazi mwanamke ana haki ya walau wiki kumi na mbili (siku 84) za likizo ya uzazi na kuendelea kupata mshahara wake.
Atapata walau siku 100 za likizo ya uzazi endapo amejifungua watoto zaidi ya mmoja (mapacha). Pia ana haki ya kupata siku nyingine 84 za likizo hiyo endapo mtoto wake atafariki ndani ya mwaka wake wa kuzaliwa. sawa na kifungu 33(6) Cha Sheria Ya Ajira na Mahusiano Kazini
Mwajiri anatakiwa kutoa likizo ya uzazi bila ya kumkata mshahara mfanyakazi si zaidi ya mara nne kwa kipindi chote atakapokuwa na mfanyakazi huyo (Sehemu ya 33 ya shereia ya kazi na mahusiano).
Mwanamme nae anayo haki ya mapumziko ya siku tatu (3) pindi mke wake wa ndoa anapojifungua mtoto. Mwajiri anawajibika kutoa likizo ya malipo kwa vipindi vine tu vya likizo ya uzazi kwa mfanyakazi. kulingana na Kifungu cha 34 cha Sheria Ya Ajira na Mahusiano kazini(Employment and Labour Relation Act)
Kama mfanyakazi ananyonyesha mtoto, mwajiri atalazimika kumruhusu mfanyakazi kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi kwa jumla ya mpaka masaa mawili kwa siku.
Mshahara Mfanyakazi atapata mshahara wake kamilifu kipindi awapo katika likizo ya uzazi. Malipo haya hulipwa na mwajiri (Sehemu ya 33 ya sheria ya kazi na mahusiano, 2004). 

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)