Usalama wa Ajira Kwa Mfanyakazi Mwajiriwa
Usalama wa Ajira
Hati ya Maandishi ya Ajira
Sheria za kazi za Tanzanian zinataka mfanyakazi apewe hati ya maandishi ya
majukumu yake ya kazi anapoanza kazi Taarifa hizo ni:
(a) jina, umri, anuani ya
kudumu na jinsia ya mfanyakazi;
(b) mahali alipoajiriwa;
(c) kazi zake;
(d) tarehe
ya kuanza;
(e) muundo na muda wa mkataba;
(f) kituo cha kazi;
(g) masaa ya kazi;
(h) ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu;
na (i) na kitu kingine kilichotajwa. Kama taarifa zote hizi zilizotajwa zimeelezwa
kwenye mkataba wa maandishi na mwajiri amempa mfanyakazi mkataba huo,
mwajiri anaweza asitoe maelezo haya tena.(Sehemu ya 15 ya sheria ya kazi na
mahusiano kazini, 2004).
Mkataba wa kazi wa kipindi maalumu
Kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania, ni marufuku kuajiri mfanyakazi kwa
kipindi cha muda maalumu ulio tajwa kwa kazi zenye asili ya kudumu.
Mkataba
na mfanyakazi utakuwa wa aina kati ya zifuatazo-
(a) mkataba kwa kipindi cha
muda usiotajwa;
(b) mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za
wataalamu na mameneja
(c) mkataba wa kazi maalumu. Hakuna sehemu yeyote
kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004 inayo toa maelezo juu
ya kuendeleza mkataba au muda wa juu wa mkataba wa kipindi maalumu (Sehemu
ya 14 ya sheria za Ajira na mahusiano Kazini).
Kipindi cha majaribio kazini
Sheria za kazi hazisemi wazi ni kwa muda gani mfanyakazi atakuwa katika
majaribio kazini chini ya mwajiri wake. Hata hivyo sehemu ya 35 ya sheria za kazi
na mahusiano, 2004 inatamka japo si wazi sana kwamba Mafanyakazi mwenye
chini ya miezi 6 kazini iwapo ataachishwa kazi hawezi kulalamika kuwa
ameachishwa kwa hila.
Kuachishwa kazi kazi kusiko kwa haki
Itakuwa si halali kisheria kwa mwajiri kusitisha ajira ya mfanyakazi bila ya
kufuata haki.
(2) Kusitishwa kwa ajira na mwajiri si kwa haki ikiwa mwajiri atashindwa
kuthibitisha -
(a) kwamba sababu za kusitisha ni halali;
(b) kwamba sababu ni sababu ya haki -
(i) inayohusiana na mwenendo wa mfanyakazi, uwezo au kuendana; au
(ii) inayohusiana na mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri; na
(c) kwamba ajira
ilisitishwa kwa kufuata taratibu za haki.
Haitakuwa sababu ya haki kusitisha
ajira ya mfanyakazi-
(a) kwa sababu kwamba-
(i) amefichua taarifa ambazo
mfanyakazi ana haki au anatakiwa kufichua kwa mtu mwingine chini ya Sheria hii
au Sheria nyingine;
(ii) ameshindwa au amekataa kufanya kitu chochote ambacho mwajiri hawezi
kisheria kuruhusu au kumtaka mfanyakazi kufanya;
(iii) ametekeleza haki yoyote
iliyotolewa kwa makubaliano, Sheria hii au sheria yoyote nyingine;
(iv) amejiunga
au alijiunga kwenye chama chochote cha wafanyakazi; au
(v) ameshiriki katika
kazi halali za chama cha wafanyakazi, ikujumuisha mgomo halali;
(b) kwa sababu-
(i) zinahusiana na ujauzito;
(ii) zinahusiana na ulemavu; na
(iii) ambazo ni za kibaguzi .
(4) Katika kuamua kama usitishwaji na mwajiri ni wa haki,
mwajiri, msuluhishi au Mahakama ya Kazi italazimika kutilia maanani
kanuni za utendaji mzuri zilizotangazwa chini ya sheria ya kazi
Nafuu ya kuachishwa kazi kusikokuwa kwa haki
Ikiwa msuluhishi au Mahakama ya Kazi imeamua kuwa usitishwaji wa ajira
ulikuwa si wa haki, msuluhishi au Mahakama inaweza kumwamuru mwajiri
(a) kumrudisha mfanyakazi kuanzia tarehe ambayo mfanyakazi aliachishwa kazi
bila kupoteza mshahara wakati ambao mfanyakazi hakuwepo kazini kwa sababu za
kuachishwa kusiko kwa haki; au
(b) kumwajiri upya mfanyakazi katika masharti ambayo msuluhishi au Mahakama
inaweza kuamua; au
(c) kumlipa mfanyakazi fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na miwili.
Kinua mgongo
“kiinua mgongo” maana yake kiasi cha mshahara wa angalau siku 7 kwa kila
mwaka ulioisha wa utumishi wa moja kwa moja na huyo mwajiri mpaka kwa
kiwango cha juu cha miaka kumi.
(2) Mwajiri atatakiwa kumlipa kiinua mgongo wakati wa kusitisha ajira ikiwa-
(a) mfanyakazi amemaliza miezi 12 ya utumishi wa moja kwa moja na mwajiri; na
(b) kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (3), mwajiri amesitisha ajira.
(a) katika usitishwaji kwa sababu za utendaji mbovu;
(b) kwa mfanyakazi ambaye amechishwa kwa sababu za uwezo, kutoendana au
mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri lakini ambaye atakataa bila sababu za msingi
kukubali ajira mbadala na mwajiri huyo au mwajiri mwingine.
(4) Malipo ya kiinua mgongo chini ya kifungu hiki hayataathiri haki nyingine za
mfanyakazi za kulipwa kiasi kingine kilipwacho chini ya Sheria hii au sheria
nyingine zilizoandikwa Kusafirishwa kwenda mahali pa kuajiriwa
Kusafirishwa baada ya kuachishwa kazi.
Kama mkataba wa mfanyakazi umesitishwa katika mahali ambapo sipo
mfanyakazi alipoajiriwa, mwajiri atatakiwa aidha,
(a) kumsafirisha mfanyakazi na vitu vyake kwenda sehemu aliyoajiriwa;
(b) kulipa gharama za usafirishaji wa mfanyakazi kwenda mahali alipoajiriwa; au
(c) kumlipa mfanyakazi posho ya usafiri kwenda sehemu aliyoajiriwa na posho
ya gharama kwa kila siku wakati wa kipindi, kama kipo, kati ya tarehe ya
kusitishwa kwa mkataba na tarehe ya kumsafirisha mfanyakazi na familia yake
kwenye sehemu aliyoajiriwa.
(2) Posho iliyotajwa chini ya sheria hii itakuwa sawasawa na angalau nauli ya basi
kwenda kituo cha basi kilicho karibu na sehemu ya kuajiriwa.
Sababu za kufukuzwa kazi kwa haki
(a) Kutoa siri za ofisi
(b)Kushindwa kutunza kumbukumbu za ofisi
(c) Utovu wa nidhamu mahali pa kazi kwa mwajiri wako na watumishi wengine
(d)Utoro kazini wa zaidi ya siku tatu nk.
Comments
Post a Comment