kiongozi au mtumishi wa umma kuorodhesha mali anazomiliki

SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NO. 13 YA 1995
kifungu cha 9 (1) (a) na (h) cha Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma Kiongozi au mtumishi wa umma atatakiwa kuorodhesha mali zake na mali anazomiliki kwa pamoja na mke au mume wake, na pia mali za watoto wenye umri ulio chini ya miaka kumi na nane ambao hawajaoa au kuolewa. Rasilimali zinazotakiwa kutajwa ni pamoja na zifuatazo:- 
(a) Fedha taslimu na amana katika benki au taasisi nyingine ya fedha; 
(b) Hawala za Hazina (Treasury Bills) na nyinginezo za dhamana maalum zinazotolewa au kudhaminiwa na serikali au vyombo vya serikali; 
(c) Faida itokanayo na fedha iliyowekwa akiba katika benki,chama cha ujenzi au taasisi nyingine ya fedha; 
(d) Mgao wa fedha kutokana na fungu la rasilimali ya kampuni (stocks)au hisa za kiongozi wa umma katika kampuni au shirika lolote; 
(e) Maslahi katika chombo cha biashara kisichokuwa na mkataba na serikali, na kisichokuwa na au kisichotawala amana zinazouzwa bayana na vyombo vya umma; 
(f) Mashamba ya kibiashara na ya matumizi binafsi; 
(g) Mali halisi zisizohamishika,kwa mfano nyumba au majengo mengine; 
(h) Rasilimali zinazoleta faida ambazo zinatakiwa kutajwa na zinamilikiwa kwa mbali.

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)