MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)
MAKOSA YA JINAI YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)
sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai Kifungu 148(5)
Afisa polisi msimamizi wa kituo cha polisi au mahakama
ambako mtuhumiwa ameletwa au amehudhuria, haitatoa dhamana kwa
mtu huyo iwapo:–
(a) mtu huyo anashitakiwa kwa:–
(i) mauaji, uhaini, ujambazi wa kutumia silaha, au unajisi wa mtoto;
(ii) usafirishaji haramu wa madawa ya kulevya
kinyume cha Sheria ya Madawa ya Kulevya na
Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Madawa ya
Kulevya, lakini haihusu mtu aliyeshitakiwa kwa
kosa la kukutwa na madawa ambayo kwa
kuzingatia mazingira yote ambako kosa
lilitendeka, haikuwa kwa makusudi ya
usafirishaji au kibiashara;
(iii) kosa linalohusisha heroini,kokeini, opiamu
iliyotayarishwa opiamu popi (papava
setijeramu), majani ya popi, mmea wa koka,
majani ya koka,kanibisi sativa au kanibisi resini
(Heipu ya India), methakyolani (mandraksi),
kata edulisi (khati) au dawa nyingine ya kulevya
au kitu cha saikotropiki kilichooreshwa kwenye
jedwali la Sheria hii ambayo ina thamani
iliyothibitishwa na Kamishina wa Kamisheni ya
Taifa ya Uratibu wa Uthibiti wa Madawa,
inayozidi shilingi milioni kumi;
(iv) ugaidi dhidi ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya
mwaka 2002;
(v) usafirishaji fedha haramu kinyume na Sheria ya
Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Fedha ya
mwaka 2006;
(b) inaonekana kwamba mtuhumiwa hapo awali aliwahi
kuhukumiwa kwa kifungo cha miaka inayozidi mitatu;
(c) inaonekana kuwa mtuhumiwa hapo awali aliwahi
kupewa dhamana na mahakama na alishindwa kutiii
masharti ya dhamana au alitoroka;
(d) inaonekana na mahakama kwamba ni muhimu kwa
mtuhumiwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya ulinzi
au usalama wake;
(e) kosa ambalo mtu anashitakiwa nalo linahusisha fedha
halisi au mali yenye thamani inayozidi shilingi milioni
kumi isipokuwa kama mtu huyo ataweka dhamana ya
fedha taslim au mali nyingine inayolingana na nusu ya
kiasi au thamani ya fedha halisi au mali iliyohusika na
inayobaki imewekewa dhamana:
Isipokuwa kwamba pale mali inayowekwa dhamana ni
mali isiyohamishika, itatosha kuweka hati miliki, au iwapo hati
miliki haipo ushahidi mwingine wowote utakaoiridhisha
mahakama kuthibitisha uwepo wa mali; isipokuwa masharti
haya hayatumika kwa dhamana ya polisi.
Comments
Post a Comment