MASHARTI YA DHAMANA YA POLISI KULINGANA NA SHERIA
MASHARTI YA DHAMANA YA POLISI KULINGANA NA SHERIA.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa Ya Jinai Kifungu 66.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa Ya Jinai Kifungu 66.
(a) anaahidi kwa maandishi kuhudhuria mbele ya mahakama iliyotajwa katika muda na mahali
palipotajwa, au katika muda mwingine na mahali kama atakavyoarifiwa na afisa polisi;
(b) anaahidi kwa maandishi kuzingatia masharti yatakayotajwa kuhusiana na mwenendo wake wakati ameachiwa kwa dhamana, masharti yasiyohusiana na utoaji wa dhamana, kuweka fedha au kutaifisha fedha;
(c) mtu mwingine anayekubalika na afisa polisi anakiri kwa maandishi, kwamba anamfahamu mtu anayeshitakiwa na anamtambua kuwa ni mtu anayewajibika ambaye anaweza kuhudhuria mahakamani kujibu mashitaka;
(d) mtu anayeshitakiwa, au mtu mwingine anayekubalika kwa afisa polisi, anaingia kwenye makubaliano, akiwa na dhamana au bila dhamana, kutaifishwa kiasi cha fedha iliyotajwa iwapo mtu aliyeshitakiwa atashindwa kuhudhuria mahakamani kujibu mashitaka; au
Comments
Post a Comment