SABABU ZINAZOWEZA SABABISHA KUNYIMWA DHAMANA KUTOKA POLISI
SABABU ZINAZOWEZA SABABISHA KUNYIMWA DHAMANA KUTOKA POLISI
Kukataa kutoa
dhamana ya polisi.
Kulingana na Sheria Ya Mwenendo Wa Makosa Ya Jinai Kifungu 67.-
(1) Pale afisa polisi anakataa kutoa dhamana atalazimika
kurekodi kwa maandishi sababu za kukataa huko.
(2) Pale afisa polisi anakataa, chini ya kifungu cha 64, kutoa
dhamana kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa, au anatoa dhamana lakini
mtu huyo hawezi au hataki kufuata, au kupanga mtu mwingine
kufuata, masharti yoyote ambayo dhamana imetolewa kwayo, mtu
huyo atalazimika kupelekwa mbele ya hakimu kushughulikiwa kwa
mujibu wa sheria mapema iwezekanavyo na si zaidi ya kikao cha
kwanza cha mahakama katika sehemu ambayo inawezekana
kumpeleka mtu huyo kwa dhumuni hilo.
(3) Mtu anayesubiri kwenye mahabusu kupelekwa mbele ya
hakimu kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) anaweza, katika muda
wowote, kumuomba afisa polisi kumpatia nyenzo kwa ajili ya kufanya
maombi ya dhamana kutoka kwa hakimu na, kama anafanya hivyo,
afisa polisi atalazimika, ndani ya saa ishirini na nne, au katika muda
mwingine wa kutosha kadri inavyowezekana baada ya kufanya
maombi, kumpeleka mbele ya hakimu.
Comments
Post a Comment