VIGEZO VYA KUTOA DHAMANA POLISI


VIGEZO VYA KUTOA DHAMANA POLISI
Kulingana na Sheria ya Mwenendo wa Makosa Ya Jinai Kifungu 65. 

Mambo ya kuzingatia katika utoaji wa dhamana mtu akiwa polisi unaofanywa na afisa polisi kwa mtu anayeshitakiwa kwa kosa ni:–

(a) uwezekano wa mtu kuhudhuria mahakamani kuhusiana na kosa kama atapewa dhamana, hii ni kusema:–
(i) historia yake na mshikamano wake na jamii au makazi, ajira na hali ya kifamilia na rekodi yake
ya polisi, kama inajulikana, na
(ii) mazingira ambao kosa lilitendeka, asili na ukubwa wa kosa, uzito wa ushahidi dhidi ya mtu
huyo na taarifa nyingine zinazohusiana na uwezekano wake wa kutoroka;

(b) maslahi ya mtu huyo, hii ni kusema–
(i) kipindi ambacho mtu huyo anaweza kulazimika kuwa mahabusu kama dhamana itakataliwa, na
masharti ambayo atashikiliwa mahabusu;
(ii) mahitaji ya mtu kuwa huru akijitayarisha kuhudhuria mbele ya mahakama, kupata ushauri
wa kisheria na kwa madhumuni mengine; au
(iii) umuhimu wa mtu huyo kupata hifadhi ya mwili, hata kama umuhimu huo unajitokeza kwa
sababu ya kutojiweza kutokana na ulevi, maumivu au matumizi ya madawa au unatokana
na sababu zingine; na
(c) hifadhi ya jamii, hii ni kusema, uwezekanao wa mtu huyo kuingilia ushahidi kwa kuwatisha mashahidi au kuzuia uchunguzi wa polisi kwa jinsi yoyote ile.

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)