MAKOSA YA KISHERIA YAHUSUYO IMANI, dini au dhehebu



MANENO YANAYOUDHI AU KUKEJERI DINI AU IMANI YA WATU WENGINE


Kanuni ya Adhabu Kifungu 129. Mtu yeyote ambaye kwa dhamiri hasa ya kumuudhi mtu yeyote juu ya imani yake ya dini akatamka maneno yoyote au akafanya sauti yoyote itakayosikiwa na mtu huyo au akafanya ishara mbele ya mtu huyo au akaweka kitu machoni pa mtu huyo, mtu afanyae hivyo amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja.


unaruhusiwa kuhubiri au kueneza au kufanya mikutano au mihadhara ya dini au injili lakini huruhusiwi kukejeri kubeza au kudhalilisha dini au imani ya mtu mwingine, ukifanya hivyo adhabu yake ni kifungo,


unashauri na mimi kuwa ni haki yako yako ya kueneza imani yako na kuwahubiri wengine lakini hakikisha maneno yako au vitendo vya havidhalilishi, kukebehi imani za watu wengine


Kanuni ya Adhabu KIfungu 125. Mtu yeyote ambaye atavunja, kuharibu au kuchafua mahali popote pa kuabudia a kitu chochote kinachoitakidiwa kitakatifu na watu wa aina yoyote kusudi la kusasfihi dini ya aina yoyote ya watu au kwa kujua kwamba watu wa aina Fulani huenda wakafikiria uvunjaji, uharibifu na uchafuaji huo kuwa ni usafihi kwa dini yao mtu huyo amekosa kosa dogo,






uhuru una mipaka yake(clawback clause) maana uhuru ukiwa hauna mipaka unaweza leta madhara( when the right of an individual is not limited then is likely to be abused.

Mfano halisi ni shauli la kesi ya


Dibagula v Republic (Criminal Appeal No. 53 of 2001) [2003] TZCA 1 (14 March 2003)


"Yesu si Mwana wa Mungu, ni jina la mtu kama mtu mwingine tu."

Comments

Popular posts from this blog

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)