SABABU ZA KISHERIA ZINAZOANGALIWA NA MAHAKAMA KATIKA KUTOA TALAKA
SABABU YA KUTOA TALAKA MAHAKAMANI
Kabla ya kupeleka shauri au maombi(petition) mahakamani
ya talaka, mwanandoa husika hana budi kufuata au
kuzingatia hatua zifuatazo;
a) kufungua au kupeleka malalamiko
kwenye
Baraza la Usuluhishi la Ndoa kwa mfano
Bakwata, kanisani,Ustawi wa Jamii au
Baraza la Kata.
b) Baraza litasikiliza, na endapo litashindwa
mapatano au muafaka kati ya wanandoa
hao,
basi baraza litatoa cheti ambacho
kitaeleza kuwa limeshindwa kusuluhisha
mgogoro wa ndoa na kuomba
mahakama kuendelea kutoa talaka.
c) Baada ya mwanadoa mmoja kupata cheti
hicho basi atatakiwa atayarishe madai ya
talaka akionyesha kuwa kulikuwa na ;-
Ndoa halali,
Kuna mgogoro kati yao,
watoto,
Mali walizochuma wakati wa ndoa yao,.
Muombaji huyo ataiomba mahakama hiyo itoe amri
ya
talaka,
mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa nguvu
za pamoja,mamlaka ya kukaa na watoto na
matunzo yao,gharama za madai / shauri.
Ili mahakama itoe talaka sababu kadha huangaliwa
na mahakama.
Sababu hizo ni mambo ambayo
yatakayofanya ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi
kwamba haiwezi kurekebishika tena(marriage has been broken beyond the repair, kulingana na Kifungu 107 cha Sheria Ya Ndoa Ya Mwaka 1971 mambo hayo ni
kama ifuatavyo;
a) Ugoni; hii ni zinaa ambayo hufanywa na
mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana.
Hii hutokea ambapo mwanaume ana mke wake au
mwanamke ana mume wake, hivyo mmoja wapo
anamwacha mke/mume na kufanya zinaa na mtu
mwingine.
b) Ukatili; ukatili ni kuumiza nafsi nyingine, kuharibu
mwili au kuwa na hofu ya kuumizwa.
c) Kulawiti; kulawiti ni kumwingilia mtu kinyume na
maumbile,
d) Kichaa; ni kutokuwa na akili timamu, na hali hii
lazima iwe imethibitishwa na madaktari bingwa wa
akili.
e) Kuzembea wajibu kwa makusudi; haya ni
majukumu ya mume, majukumu hayo ni kama
haya; kumtunza mke kwa kumpa chakula, malazi na
mavazi.
f) Uasi Ni hali ya mke au mume kuhama nyumba ya
ndoa na kwenda kuishi mahala pengine bila sababu
yoyote ya msingi,
g) Kutengana; kukaa mbalimbali kwa mume na mke
kwa muda wa miaka isiyo pungua mitatu, kutengana
kwao ni sababu tosha ya talaka.
h) Dhana ya kifo; hii ni hali ambayo mmoja wa wana
ndoa amekufa, na hii hutokea iwapo mojawapo
hataonekana / ametoroka kwa muda mrefu, kama
miaka 5. Hapo mahakama hutoa tangazo kuwa
fulani amekufa.
i) Kifungo; hii ni hali ambayo mume au mke ametenda
kosa la jinai na ametiwa hatiani na mahakama
imemfunga miaka 5 au maisha basi mahakama
inaweza kutoa talaka kwa mwombaji.
j) Tofauti za imani za kidini, endapo mwanandoa
mmoja atabadili dini basi ni sababu tosha ya kuomba
mahakama ivunje ndoa na kutoa talaka.
Comments
Post a Comment