SHERIA ILIYOMPA RAISI MAGUFURI MAMLAKA YA KUWASAMEHE PAPI KOCHA NA BABU SEYA




Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 45 (1) (a-d) imempa mamlaka Rais kusamehe wafungwa kwa masharti, adhabu yote au sehemu ya adhabu aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote, ambayo alistahili kupewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


(a) Raisi ana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) Raisi ana mamlaka Ya kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) Raisi ana mamlaka kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) Raisi ana mamlaka kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.

Kanuni ya Adhabu Kifungu 3(5) uwezo wowote wa Rais kutoa msamaha wowote au kupunguza adhabu au kubadilisha adhabu yote au sehemu ya adhabu au kuahirisha utimizaji wa hukumu yoyote iliyokwishatolewa au itakayotolewa






kwa maelezo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria Ya Kanuni Ya Adhabu raisi Ana haki wa kuwasamehe na kuwafutia adhabu au kifungo Babu sea na wenzake, pia sheria haitaja kosa imesema tuu kuwa Raisi ana mamlaka hayo

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)