TOFAUTI YA KISHERIA ILIYOPO KATI YA KUTENGANA NA TALAKA( Separation and divorce) KULINGANA NA SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971
TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA
KUTENGANA
Kutengana si talaka. Kutengana maana yake ni hali ambayo mke na mume hukaa mbalimbali. Kukaa mbalimbali au kutengana kwaweza kuwa kwa mapatano kati ya wanandoa hao au kutengana kwaweza kuwa kwa amri ya mahakama. Mahakama itatoa amri hiyo endapo mmoja wao atapeleka maombi mahakamani. Faida ya kutengana wote au mmoja wao waweza au aweza kutambua makosa na baadaye kukata shauri kurudiana au kuishi tena.
Kutengana kwa mapatano,
Ni kutengana kwa hiari yao wenyewe bila shuruti.
Mapatano hayo yaweza kuwa ya maandishi au ya mdomo. Mambo kadha
yaweza kuzingatiwa wakati wa makubaliano kama;
heshima kwa kila mmoja, matumizi / matunzo,watoto
kama wapo watakaa na nani, mali ya pamoja je
itatunzwa namna gani na kutobughudhiana.
Kutengana kwa amri ya mahakama,
hii ni hali ya
mume na mke kutengana kwa amri ya mahakama
na mahakama imeridhika kuwa ndoa imevunjika.
Ushahidi wa kuwa ndoa imevunjika ni ushahidi
ambao unaweza kutolewa mbele ya mahakama
kunapokuwepo na maombi au shauri la talaka.
TALAKA
Talaka ni ruhusa au amri ya mahakama ya kisheria
ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha
mwenzake.
Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka ni
mahakama tu. Mahakama hiyo itatoa talaka kwa
ndoa ambayo imedumu kwa muda wa miaka miwili
au zaidi. Mahakama inaweza kutoa talaka kwa ndoa
ambayo haijafikisha muda huo endapo mlalalmikaji
atatoa sababu za msingi mahakamani
Comments
Post a Comment