HAKI ZA MPANGAJI

uhusiano uliopo kati ya mwenye nyumba na mpangaji ni ule wa kimkataba(contractual relation), mahusiano haya ya kimkataba yanaweka wajibu kwa mpangaji na mwenye nyumba wake, lakini pia mpangaji na wmenye nyumba kila mmoja ana haki yake na jukumu lake kimkataba

Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999(Land Act), Sheria Ya Usajili wa Ardhi (Land Registration Act) zinatambua majukumu na haki za mpangaji wa nyumba
Jukumu na Wajibu wa Mpangaji katika Nyumba ni
1.Kulipa Kodi
2.Kutoharibu miondombinu ya nyumba
3.Kutunza mazingira ya Nyumba na mazingira ya nyumba
4.Haruhusiwi kukata miti ya mwenye nyumba

haki za mpangaji ni pamoja na kuishi bila kubughudhiwa (quite enjoyment of the leased premise) kama ilivyo elezwa na kifungu 88(1)(d) cha sheria ya Ardhi ya mwaka 1999.
kuishi nyumba iliyokatika hali nzuri ( fit for human habitation) ni jukumu la mwenye nyumba kurekebisha na kufanyia marekebisho(repair) nyumba aishiyo mpangaji wake. endapo miezi sita ikapita bila kufanya marekebisho bhasi mpangaji anahaki ya kuhama na kuvunja mkataba kama inavyoelezwa katika kifungu cha 88(1)(e) Sheria Ya Ardhi Ya Mwaka 1999
kuishi kwa uhuru wa kutumia nyumba au nyumba aliyopanga pasipo kuingiliwa tena na mwenye nyumba( exclusive possession)

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)