KOSA LA KUAZIMISHA NA
KUAZIMISHA VYETI
Hili ni kosa la jinai
ambapo anaazimisha cheti kwa mtu mwingine akiwa na lengo la kukitumia kwa
manufaa Fulani, hili kosa linaadhibiwa kisheria baada ya mtuhumiwa kupatikana
na hatia kuwa aliazimisha cheti chake kitumike na mtu mwingine kinyume cha
sheria Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 373, kinaeleza kama ifuatavyo
’’Mtu
yeyote ambaye, akiwa yeye ndiye aliyepewa nyaraka yoyote iliyotolewa na mamlaka
halali ambapo amedhibitishwa kuwa ni mwenye sifa zozote zinazotambulika na
sheria kwa madhumuni yoyote, au kuwa ni mwenye ofisi yoyote, au kuwa na haki ya
kufanya kazi ya taaluma yoyote, biashara, au kuwa na haki yoyote au upendeleo,
au kwa kutumia cheo chochote au hadhi, anauza, anatoa au anaazima nyaraka hiyo
kwa mtu mwingine kwa dhamira kwamba huyo mtu mwingine anaweza kujiwakilisha
kuwa yeye ndiye mtu aliyetajwa katika nyaraka
hiyo, atakuwa anatenda kosa’’
Sheria imeenda mbali
zaidi na kutambua kuwa hata aliyeazima cheti hicho anakuwa ametenda kosa la
jinai kulingana na Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 371
‘’Mtu
yeyote ambaye anatoa nyaraka yoyote, ambayo imetolewa na mamlaka halali kwa mtu
mwingine na kwamba huyo mtu mwingine anashuhudiwa kuwa ni mtu mwenye sifa
inayotambulikana na sheria kwa madhumuni yoyote, au ni mwenye ofisi yoyote, au
ni mwenye haki ya kutumia utaalam wowote, biashara au kazi au kuwa anastahili
kupata haki au upendeleo wowote, au kutumia cheo au nafasi yoyote, na
akajionyesha yeye kuwa ndie huyo mtu aliyetajwa katika hati hiyo, atakuwa
anatenda kosa la namna hiyo na atawajibika kwa adhabu kama vile ameghushi
nyaraka’’.
Comments
Post a Comment