KOSA LA KUFANYA MAPENZI
KINYUME NA MAUMBILE
Kulingana na watu kuwa
wabunifu wa kutenda dhambi na kuongezeka kwa maarifa, tafiti zinaonesha ukatili
wa jinsia unaongezeka na idadi ya talaka pia zinaongezeka kwa sababu ya watu
kufanya kamchezo kanakojulikana kama kuruka ukuta na kusukuma tope yaani
kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Kulingana na sheria
yetu ya Kanuni Ya Adhabu (Penal Code) kifungu cha 154 kufanya mapenzi kinyume
cha maumbile ni kosa la jinai na adhabu
yake ni kifungo cha maisha.
Mtu yeyote ambaye
anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au, anamuingilia mnyama kimwili
au anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye
mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile, atakuwa ametenda kosa, na
atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo
kisichopungua miaka thelathini .
Lakini Ikiwa kosa limetendwa dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi,
mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha hii ni kulingana na kanuni
ya Adhabu(Penal Code) Kifungu 154(2)
Sheria imeenda mbali
zaidi na kutoa adhabu kwa Kujaribu kujamiiana kinyume cha maumbile na ukipatwa
na hatia ni adhabu ya kifungo cha miaka 20 jera hii ni kulingana na Kanuni Ya
Adhabu kifungu 155.
Kulingana na Sheria ya
Ndoa ya Mwaka 1971(The Law Of Marriage
Act) kifungu cha 107, kinaeleza kitendo cha kujamiana kinyume na maumbile
(sexual pervasion) ni ushahidi tosha kuwa ndoa imefikia sehemu mbaya hivyo
mwanandoa anaweza kudai talaka akieleza hicho kitendo kuwa ni ushahidi kuwa
ndoa imefikia pabaya hivyo anaweza tumia hicho kigezo kudai talaka.
Tunaposema ndoa kufika
pabaya tunamaana ndoa kufika mahali ambapo wanandoa hawawezi kuendelea kuishi
pamoja kama mume na mke; yaani muathilika hawezi tena kuendelea kuvumilia ile
hali. Hata kama ndoa hiyo inasiku moja tu baada ya kufungwa hayo ni kulingana
na kifungu 99 cha sheria ya ndoa, ilitokea katika shauri la case ya corbet v,
corbet wanandoa walifunga ndoa walipofika nyumbani akamkuta mwenza ni jinsia
moja sawa na yeye, kesho yake akaenda mahakamani
ndoa ikavunjwa.
Hivyo basi kwa mujibu
ya sheria ya kanuni ya adhabu kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile
adhabu yake ni kifungo cha maisha au miaka 30 au miaka 20, lakini kwa mujibu wa
sheria ya ndoa 1971 mahakama inatoa
taraka kwa wanandoa endapo muathilika atalalamika
Comments
Post a Comment