KOSA LA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI

JE UNAJUA KUWA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI KWA LENGO LA KUDANGANYA NI KOSA LA JINAI
Watu wengi wamekuwa wakitenda kosa la kuhamisha mipaka kwa lengo la kudanganya na kujiongezea ukubwa wa maeneo yao wanayomiliki, lakini hili jambo limekuwa mara nyingi limechukuliwa kama kosa la madai, lakini kulingana sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 linatumbuliwa kuwa ni kosa la jinai. Kifungu hicho kinaeleza kama ifuatavyo.
’’ Mtu yeyote ambaye, kwa kunuwia na isivyokuwa halali na kwa nia ya kudanganya, anaondosha au anafuta kitu chochote au alama ambayo iliyowekwa kihalali kama alama ya mpaka wa ardhi yoyote atakuwa anatenda kosa  la jinai’’
ADHABU KWA ALIYEHAMISHA MIPAKA

Adhabu yake kulingana na Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 ni Miaka mitatu endapo mtuhumiwa atakuwa amepatikana na hatia. Hivyo mnashauriwa mridhike na mipaka ya maeneo yenu ili kuepuka adhabu hii inayotolewa na sheria.

Comments

Popular posts from this blog

Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)