KOSA LA KUVAMIA ARDHI/ CRIMINAL TRESPASS NA ADHABU YAKE KULINGANA NA SHERIA ZETU
KOSA LA KUINGIA KWA JINAI (CRIMINAL TRESPASS) AU UVAMIZI WA
ARDHI
Kanuni ya Adhabu
kifungu cha 299 kinaeleza kuwaMtu yeyote ambaye Isivyokuwa halali anaingia
ndani ya mali inayomilikiwa na mwingine kwa kusudi la kutenda kosa au kumtisha,
kumtukana au kumuudhi mtu yeyote mwenye kumiliki mali hiyo au ameingia kwa
halali ndani ya mali hiyo na bila ruhusa halali akabaki humo kwa kusudi la
kumtishia, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo au kwa kusudi la
kutenda kosa. atakuwa anatenda kosa la kuingia kwa jinai
ADHABU YA KUINGIA KWA
JINAI
Adhabu yake ni kifungo
cha miezi mitatu hii ni kwa mtu aliingia isivyohalali ndani ya mali
inayomilikiwa
Ikiwa mtu ameingia ndani ya mali ilivyo halali
kwa ruhusa lakini bila ruhusa au idhini akaendelea kubaki ndani ya eneo kwa
lengo la kumtisha, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo adhabu yake
ni kifungo cha mwaka mmoja
NAMNA NYINGINE YA KUPATA
FIDIA KWA ARDHI ILIYOVAMIWA
Zingatia kuwa unaweza
kufanya kosa hili kuwa kesi au shauli la madai na ukapata fidia endapo
ukadhibitisha kuwa mvamizi huyo aliyevamia eneo lako amekusababishia madhara au
hasara yeyote kwa yeye kuvamia eneo lako unalomiki kihalali, hivyo jinsi
utakavyoweza kudhibitisha ndivyo utapewa fidia nzuri zaidi.
Comments
Post a Comment