KOSA LA KUVUNJA NYUMBA KULINGANA NA SHERIA YETU
KOSA
LA KUVUNJA NYUMBA (HOUSEBREAKING & BULGRALY)
Kosa
hili la jinai linahusisha mtu kuingia na kuvunja katika jengo lolote
linalotumika kama makazi ya kuishi binadamu kwa dhamira ya kutenda kosa
Yafuatayo
yanahusisha kosa la kuvunja nyumba
Ø (1) Mtu ambaye anavunja sehemu
yeyote,, iwe nje au ndani ya jengo, au anafungua mlango uliyofungwa, anavuta,
anasukuma au anainua, au kwa namna nyingine yoyote, mlango wowote, dirisha,
kifungio chochote, kilango cha dari au kitu kingine, ambavyo vimekusudiwa kufunga
au kuziba uwazi katika jengo hilo, au uwazi unaotoa njia ya kutoka sehemu moja
ya jengo mpaka nyingine, anachukuliwa kuwa amevunja jengo hilo.
Ø (2) Mtu anachukuliwa kuingia
ndani ya jengo mara tu ambapo sehemu yoyote ya mwili wake au sehemu yoyote ya
chombo chochote alichokitumia kipo ndani ya jengo hilo.
Ø (3) Mtu ambaye ameingia ndani ya
jengo kwa njia za kitisho au hilo itumikayo kwa haja hiyo, au kwa kushirikiana
kwa hila na mtu yeyote aliyemo ndani ya jengo hilo, au kwa kula njama na mtu
yeyote aliyeko katika jengo au kwa kupenya katika bomba la kutokea moshi au
sehemu jingine la jengo hilo, ambalo daima limekaa wazi kwa mahitaji yoyote ya
lazima, lakini kwa kawaida halikukusudiwa kutumika kama njia ya kuingilia,
anachukuliwa kwamba amevunja na kuingia ndani ya jengo hilo.
ADHABU YAKE
Ø Kosa hili la jinai likifanyika
mchana inaitwa housebreaking adhabu yake endapo mtuhumiwa atakutwa na hatia ni
kifungo cha miaka 12
Ø Likifanyika usiku adhabu yake ni
miaka 20 linajulikana kama burglary
Ø Kosa la kuingia na kutenda kosa
bila ya kuvunja nyumba atawajibika kwa
kifungo cha miaka 10 endapo ikafanyika
mchana, likifanyika usiku Adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 kulingana na Kanuni
ya Adhabu Kifungu cha 295.
Comments
Post a Comment