Posts

Haki za Raia anapokuwa amekamatwa na polisi

Image
Raia una haki ya kumwomba  askari ajitambulishe kwako. 1.Mwulize jina lake 2.Mwulize namba  yake ya uaskari 3.Raia ana haki ya  kujulishwa kwanini  anatiliwa mashaka  ama kukamatwa. 4.Raia ana haki ya  kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu  anakofanyia kazi  kwamba ama amekamatwa na polisi  ama Taasisi ya Kuzuia  Rushwa. 5.Raia ana haki ya  kuomba na kupewa  dhamana wakati  akiwa kituo cha polisi  ama Taasisi ya kuzuia rushwa. 6.Hutakiwi kutoa  fedha kama  dhamana uwapo kituo cha polisi  ama Taasisi ya  Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo  utakayoandika. 7.Raia ana haki ya  kuwaeleza polisi ama  Maafisa wa Kuzuia  Rushwa kwamba  lolote atakalosema linaweza kutumiwa  kama ushahidi  mahakamani, na asiburuzwe kuandika  tu. 8.Raia ana haki ya  kuomba Wakili wake  awepo kituo cha polisi  ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati  anatoa maelezo yake. 9.Raia ana haki ya  kuyasoma kabla ya  kutia sahihi yake. 10.Raia ana haki ya  kudai risiti ya orodha  ya vitu vyake

NAMNA YA KUKATA RUFAA KWA KESI NA MASHAURI YA ARDHI

Image
NAMNA YA KUKATA RUFAA KWA KESI NA MASHAURI YA ARDHI Rufaa  ni  hatua  ya   kisheria  ambayo  hufikiwa  na  mhusika  katika  shauri   fulani  iwapo  hakuridhishwa  na  maamuzi. Rufaa  sio  mpaka  uwe  umeshindwa  kabisa,  hapana. Yawezekana  ukawa  umeshinda  kesi  lakini  hukuridhishwa  na kiwango   ulichoshinda.Kwa  mfano  uliomba  wavamizi  waondoke  katika  nyumba yako   na  hapohapo  wakulipe  fidia.  Mahakama  ikatoa  hukumu  kuwa  umeshinda  wavamizi  waondoke  katika  nyumba  yako  lakini  ikasema wasikulipe  fidia.  Mazingira  kama  haya  unakuwa  umeshinda  lakini  ukitaka  unaweza  kukata  rufaa  kulalamikia kutolipwa  fidia.  Kwa hoja  hii  tunaona  kuwa kumbe  kukata  rufaa  si  lazima  uwe  umeshindwa  badala  yake unaweza  kuwa umeshinda  lakini  ukawa  hukuridhishwa  na  vitu  fulani  katika  hukumu  ambavyo  unaweza  kuvikatia  rufaa  ili  navyo  uvipate. 1.AINA  ZA  RUFAA  KATIKA  MASHAURI  YA  ARDHI. Kisheria  rufaa  hutofautiana  kutokana   na  aina 

Dhania ya mwanamke na mwanaume kuchukuliwa kama wanandoa baada ya kuishi pamoja kwa mda fulani

Image
Dhana ya kuchukulia ndoa Kuna dhana inayokanushika (rebuttable   presumption) kuwa mwanamme na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria   japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.   (i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamme wameishi pamoja kwa muda wa miaka miwili au zaidi kwa mfululizo.   (ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma  unaowazunguka unawachukulia na  kuwapa heshima kama mke na mume.  (iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao  walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume  wakati walipoanza kuishi pamoja kama  umri ulikubalika kisheria.   (iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa   inayoendelea.  
Image
Vipengele gani vya kuzingatia ili wanaotaka kufunga ndoa wakubaliwe kisheria kufunga ndoa  (a) Ni lazima muungano uwe wa hiari Mume na mke wawe wameamua kuishi pamoja kwa ridhaa yao wenyewe. Hii inamaanisha kusiwe na kulazimishwa, kuhadaiwa kwa aina yoyote kwani   muungano kama huo utakuwa batili kisheria.   Ni kosa la jinai kushiriki katika shughuli ya ndoa ambayo mmoja wapo au wote wamelazimishwa kufunga ndoa.   (b) Muungano uwe ni kati ya mwanamke na mwanamme Muungano wa watu wa jinsia moja hata kama ni wa hiari muungano huo hautambuliki kisheria.   Pia mtu huhesabika mwanamke au mwanamme kutokana na   sehemu za siri alizozaliwa nazo na siyo alizozipata baadaye. Jamii inachukulia kuwa ndoa ni njia pekee   ya kujipanua, upanukaji huku ni kwa kuzaa watoto.   Kwa hali hiyo ili kupata watoto ni lazima ndoa iwe kati ya mwanamme na mwanamke. (c) Muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa kudumu Pamoja na kuwa mwanamke na