
KOSA LA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE Kulingana na watu kuwa wabunifu wa kutenda dhambi na kuongezeka kwa maarifa, tafiti zinaonesha ukatili wa jinsia unaongezeka na idadi ya talaka pia zinaongezeka kwa sababu ya watu kufanya kamchezo kanakojulikana kama kuruka ukuta na kusukuma tope yaani kufanya mapenzi kinyume cha maumbile. Kulingana na sheria yetu ya Kanuni Ya Adhabu (Penal Code) kifungu cha 154 kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha maisha. Mtu yeyote ambaye anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au, anamuingilia mnyama kimwili au anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile, atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini . Lakini Ikiwa kosa limetendwa dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha hii ni kulingana na kanuni ya Adhabu(...