MAKOSA YA JINAI YA UVIVU NA UZEMBE
MAKOSA YA JINAI YA UZEMBE NA UVIVU Sheria yetu ya kanuni ya adhabu inatambua makosa ya uvivu na uzembe kama makosa ya jinai yanayoadhibiwa kisheria, fungu la 176 ya kanuni ya Adhabu. ü Kucheza kamari kuwa ni kosa la jinai ü Kufanya umalaya ü Kufanya kitendo cha aibu mbele ya hadhara/ kufanya mapenzi mbele ya watu. ü mtu aliyeajiriwa chini ya ajira halali inayotambulika ambaye, bila udhuru halali, anapatikana akichezacheza au kufanya mzaha wakati wa muda wa kazi, atahesabiwa kuwa ni mtu mvivu na mzembe na atapaswa kulipwa faini isiyozidi shilingi mia tano au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja. ü mtu anayetangatanga au anayejiweka katika mahali popote pa hadhara kwa kuomba au kukusanya sadaka, kumtuma au kumhimiza mtoto kufanya hivyo; ü mtu anayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa namna yoyote kwa njia ya kujisingizia au hadaa; ü mtu anakayeonekana ndani au ...