Posts

kiongozi au mtumishi wa umma kuorodhesha mali anazomiliki

Image
SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NO. 13 YA 1995 .  kifungu cha 9 (1) (a) na (h) cha Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma Kiongozi au mtumishi wa umma atatakiwa kuorodhesha mali zake na mali anazomiliki kwa pamoja na mke au mume wake, na pia mali za watoto wenye umri ulio chini ya miaka kumi na nane ambao hawajaoa au kuolewa. Rasilimali zinazotakiwa kutajwa ni pamoja na zifuatazo:-  (a) Fedha taslimu na amana katika benki au taasisi nyingine ya fedha;  (b) Hawala za Hazina (Treasury Bills) na nyinginezo za dhamana maalum zinazotolewa au kudhaminiwa na serikali au vyombo vya serikali;  (c) Faida itokanayo na fedha iliyowekwa akiba katika benki,chama cha ujenzi au taasisi nyingine ya fedha;  (d) Mgao wa fedha kutokana na fungu la rasilimali ya kampuni (stocks)au hisa za kiongozi wa umma katika kampuni au shirika lolote;  (e) Maslahi katika chombo cha biashara kisichokuwa na mkataba na serikali, na kisichokuwa na au kisichotawala amana zinazouzwa bayana na vyombo vya um

KOSA LA KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA TAKWIMU KINYUME NA SHERIA YA TAWIMU

Image
SHERIA YA TAKWIMU NO.9 YA MWAKA 2015 Kifungu no. 37(2) Mtu yeyote bila mamlaka halali anachapisha au kutoa na kusambaza taarifa za takwimu ambazo kwa ufahamu wake kwa watu wengine kinyume na utaratibu wa sheria ya takwimu tofauti na utaratibu wa sheria kutoa taarifa au kuchapisha sheria huyo mtu atakuwa ametenda kosa la jinai atawajibika kulipa faini ya shiling Milion 5 au kutumikia kifungo k isichopungua mwezi kumi na mbili, au vyote kwa pamoja. kuwa makini katika kueneza na kusambaza taarifa unazozipata  kwa maelezo zaidi tembelea. Mkumbushe na rafiki yako ili nawe asije akanaswa

SABABU ZINAZOWEZA SABABISHA KUNYIMWA DHAMANA KUTOKA POLISI

Image
SABABU ZINAZOWEZA SABABISHA KUNYIMWA DHAMANA KUTOKA POLISI Kukataa kutoa dhamana ya polisi.

MASHARTI YA DHAMANA YA POLISI KULINGANA NA SHERIA

Image
MASHARTI YA DHAMANA YA POLISI KULINGANA NA SHERIA . Sheria ya Mwenendo wa Makosa Ya Jinai Kifungu 66 .  Mtu atakuwa na haki ya kupata dhamana ya polisi kama:–

VIGEZO VYA KUTOA DHAMANA POLISI

Image
VIGEZO VYA KUTOA DHAMANA POLISI Kulingana na Sheria ya Mwenendo wa Makosa Ya Jinai Kifungu 65.   Mambo ya kuzingatia katika utoaji wa dhamana mtu akiwa polisi  unaofanywa na afisa polisi kwa mtu anayeshitakiwa kwa kosa ni:– (a) uwezekano wa mtu kuhudhuria mahakamani kuhusiana na kosa kama atapewa dhamana, hii ni kusema:– (i) historia yake na mshikamano wake na jamii au makazi, ajira na hali ya kifamilia na rekodi yake ya polisi, kama inajulikana, na (ii) mazingira ambao kosa lilitendeka, asili na ukubwa wa kosa, uzito wa ushahidi dhidi ya mtu huyo na taarifa nyingine zinazohusiana na uwezekano wake wa kutoroka; (b) maslahi ya mtu huyo, hii ni kusema– (i) kipindi ambacho mtu huyo anaweza kulazimika kuwa mahabusu kama dhamana itakataliwa, na masharti ambayo atashikiliwa mahabusu; (ii) mahitaji ya mtu kuwa huru akijitayarisha kuhudhuria mbele ya mahakama, kupata ushauri wa kisheria na kwa madhumuni mengine; au (iii) umuhimu wa mtu huyo kupata hifadhi ya

MAKOSA YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES)

Image
MAKOSA YA JINAI YASIYO NA DHAMANA(NON BAILABLE OFFENCES) sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai Kifungu 148(5)  Afisa polisi msimamizi wa kituo cha polisi au mahakama ambako mtuhumiwa ameletwa au amehudhuria, haitatoa dhamana kwa mtu huyo iwapo:–  (a) mtu huyo anashitakiwa kwa:–  (i) mauaji, uhaini, ujambazi wa kutumia silaha, au unajisi wa mtoto;  (ii) usafirishaji haramu wa madawa ya kulevya kinyume cha Sheria ya Madawa ya Kulevya na Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Madawa ya Kulevya, lakini haihusu mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la kukutwa na madawa ambayo kwa kuzingatia mazingira yote ambako kosa lilitendeka, haikuwa kwa makusudi ya usafirishaji au kibiashara;  (iii) kosa linalohusisha heroini,kokeini, opiamu iliyotayarishwa opiamu popi (papava setijeramu), majani ya popi, mmea wa koka, majani ya koka,kanibisi sativa au kanibisi resini (Heipu ya India), methakyolani (mandraksi), kata edulisi (khati) au dawa nyingine ya kulevya au kitu cha saikotropiki kilichooreshwa kwenye jed

Haki za Raia anapokuwa amekamatwa na polisi

Image
Raia una haki ya kumwomba  askari ajitambulishe kwako. 1.Mwulize jina lake 2.Mwulize namba  yake ya uaskari 3.Raia ana haki ya  kujulishwa kwanini  anatiliwa mashaka  ama kukamatwa. 4.Raia ana haki ya  kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu  anakofanyia kazi  kwamba ama amekamatwa na polisi  ama Taasisi ya Kuzuia  Rushwa. 5.Raia ana haki ya  kuomba na kupewa  dhamana wakati  akiwa kituo cha polisi  ama Taasisi ya kuzuia rushwa. 6.Hutakiwi kutoa  fedha kama  dhamana uwapo kituo cha polisi  ama Taasisi ya  Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo  utakayoandika. 7.Raia ana haki ya  kuwaeleza polisi ama  Maafisa wa Kuzuia  Rushwa kwamba  lolote atakalosema linaweza kutumiwa  kama ushahidi  mahakamani, na asiburuzwe kuandika  tu. 8.Raia ana haki ya  kuomba Wakili wake  awepo kituo cha polisi  ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati  anatoa maelezo yake. 9.Raia ana haki ya  kuyasoma kabla ya  kutia sahihi yake. 10.Raia ana haki ya  kudai risiti ya orodha  ya vitu vyake