Posts

Showing posts from July, 2018

KOSA KUSHANGILIA AU KUCHOCHEA WATU WANAOTENDA UHALIFU (SOLICITATION AND INCITEMENT)

Image
JE WAJUA KUWA KUSHANGILIA AU KUCHOCHEA AU KUSHADADIA WATU WANAPIGANA AU KUTENDA UHARIFU NI KOSA LA JINAI. Pamoja na Tanzania kuwa nchi ya amani lakini pia watu wameendelea kutenda makosa ya jinai yanayo hatarisha amani bila kujua na kuchochukuliwa hatua za kisheria kwa sababu matukio haya yanafahamika lakini hayaripotiwi. Kanuni Ya Adhabu 390. Mtu yeyote ambaye anamshawishi au anamchochea mtu mwingine kutenda kosa, atakuwa anatenda kosa bila kujali kwamba ushawishi au uchochezi huo hauna madhara.
Image
KOSA LA KUAZIMISHA NA KUAZIMISHA  VYETI Hili ni kosa la jinai ambapo anaazimisha cheti kwa mtu mwingine akiwa na lengo la kukitumia kwa manufaa Fulani, hili kosa linaadhibiwa kisheria baada ya mtuhumiwa kupatikana na hatia kuwa aliazimisha cheti chake kitumike na mtu mwingine kinyume cha sheria Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 373, kinaeleza kama ifuatavyo ’’Mtu yeyote ambaye, akiwa yeye ndiye aliyepewa nyaraka yoyote iliyotolewa na mamlaka halali ambapo amedhibitishwa kuwa ni mwenye sifa zozote zinazotambulika na sheria kwa madhumuni yoyote, au kuwa ni mwenye ofisi yoyote, au kuwa na haki ya kufanya kazi ya taaluma yoyote, biashara, au kuwa na haki yoyote au upendeleo, au kwa kutumia cheo chochote au hadhi, anauza, anatoa au anaazima nyaraka hiyo kwa mtu mwingine kwa dhamira kwamba huyo mtu mwingine anaweza kujiwakilisha kuwa yeye ndiye mtu aliyetajwa katika nyaraka  hiyo, atakuwa anatenda kosa’’ Sheria imeenda mbali zaidi na kutambua kuwa hata aliyeazima cheti hicho anaku...

KOSA LA KUVUNJA NYUMBA KULINGANA NA SHERIA YETU

Image
KOSA LA KUVUNJA NYUMBA (HOUSEBREAKING & BULGRALY) Kosa hili la jinai linahusisha mtu kuingia na kuvunja katika jengo lolote linalotumika kama makazi ya kuishi binadamu kwa dhamira ya kutenda kosa Yafuatayo yanahusisha kosa la kuvunja nyumba Ø   (1) Mtu ambaye anavunja sehemu yeyote,, iwe nje au ndani ya jengo, au anafungua mlango uliyofungwa, anavuta, anasukuma au anainua, au kwa namna nyingine yoyote, mlango wowote, dirisha, kifungio chochote, kilango cha dari au kitu kingine, ambavyo vimekusudiwa kufunga au kuziba uwazi katika jengo hilo, au uwazi unaotoa njia ya kutoka sehemu moja ya jengo mpaka nyingine, anachukuliwa kuwa amevunja jengo hilo. Ø   (2) Mtu anachukuliwa kuingia ndani ya jengo mara tu ambapo sehemu yoyote ya mwili wake au sehemu yoyote ya chombo chochote alichokitumia kipo ndani ya jengo hilo. Ø   (3) Mtu ambaye ameingia ndani ya jengo kwa njia za kitisho au hilo itumikayo kwa haja hiyo, au kwa kushirikiana kwa hila na mtu yeyote aliyemo nd...

KOSA LA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI

Image
JE UNAJUA KUWA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI KWA LENGO LA KUDANGANYA NI KOSA LA JINAI Watu wengi wamekuwa wakitenda kosa la kuhamisha mipaka kwa lengo la kudanganya na kujiongezea ukubwa wa maeneo yao wanayomiliki, lakini hili jambo limekuwa mara nyingi limechukuliwa kama kosa la madai, lakini kulingana sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 linatumbuliwa kuwa ni kosa la jinai. Kifungu hicho kinaeleza kama ifuatavyo. ’’ Mtu yeyote ambaye, kwa kunuwia na isivyokuwa halali na kwa nia ya kudanganya, anaondosha au anafuta kitu chochote au alama ambayo iliyowekwa kihalali kama alama ya mpaka wa ardhi yoyote atakuwa anatenda kosa  la jinai’’ ADHABU KWA ALIYEHAMISHA MIPAKA Adhabu yake kulingana na Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 ni Miaka mitatu endapo mtuhumiwa atakuwa amepatikana na hatia. Hivyo mnashauriwa mridhike na mipaka ya maeneo yenu ili kuepuka adhabu hii inayotolewa na sheria.
Image
KOSA LA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE Kulingana na watu kuwa wabunifu wa kutenda dhambi na kuongezeka kwa maarifa, tafiti zinaonesha ukatili wa jinsia unaongezeka na idadi ya talaka pia zinaongezeka kwa sababu ya watu kufanya kamchezo kanakojulikana kama kuruka ukuta na kusukuma tope yaani kufanya mapenzi kinyume cha maumbile. Kulingana na sheria yetu ya Kanuni Ya Adhabu (Penal Code) kifungu cha 154 kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni  kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha maisha. Mtu yeyote ambaye anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au, anamuingilia mnyama kimwili au  anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile, atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini . Lakini  Ikiwa kosa limetendwa  dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha hii ni kulingana na kanuni ya Adhabu(...

KOSA LA KUVAMIA ARDHI/ CRIMINAL TRESPASS NA ADHABU YAKE KULINGANA NA SHERIA ZETU

Image
KOSA LA KUINGIA KWA  JINAI (CRIMINAL TRESPASS)  AU UVAMIZI WA  ARDHI Kanuni ya Adhabu kifungu cha 299 kinaeleza kuwaMtu yeyote ambaye Isivyokuwa halali anaingia ndani ya mali inayomilikiwa na mwingine kwa kusudi la kutenda kosa au kumtisha, kumtukana au kumuudhi mtu yeyote mwenye kumiliki mali hiyo au ameingia kwa halali ndani ya mali hiyo na bila ruhusa halali akabaki humo kwa kusudi la kumtishia, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo au kwa kusudi la kutenda kosa. atakuwa anatenda kosa la kuingia kwa jinai ADHABU YA KUINGIA KWA JINAI Adhabu yake ni kifungo cha miezi mitatu hii ni kwa mtu aliingia isivyohalali ndani ya mali inayomilikiwa  Ikiwa mtu ameingia ndani ya mali ilivyo halali kwa ruhusa lakini bila ruhusa au idhini akaendelea kubaki ndani ya eneo kwa lengo la kumtisha, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja NAMNA NYINGINE YA KUPATA FIDIA KWA ARDHI ILIYOVAMIWA Zingatia kuwa unaweza kufan...

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Image
KOSA LA KUGHUSHI VYARAKA MBALIMBALI Kanuni ya Adhabu kifungu cha 333 kinaeleza nini maana ya kughushi ikiwa ni ni kutengeneza nyaraka ya uwongo kwa nia ya kudanganya au kuhadaa. Kanuni ya Adhabu kifungu cha 335 kinaeleza kuwa. Mtu yeyote anayetengeneza nyaraka ya uwongo ambaye–  (a) anafanya nyaraka ambayo ni ya uwongo au ambayo ana sababu ya kuamini kuwa si ya kweli;  (b) anabadili nyaraka bila ya mamlaka kwa namna ambayo iwapo kubadili huko kungekuwa na mamlaka kungebadili matokeo ya nyaraka hiyo;  (c) anaingiza katika nyaraka hiyo bila ya mamlaka , wakati nyaraka hiyo inaandikwa, jambo ambalo kama lingeruhusiwa lingebadilisha matokeo ya nyaraka hiyo;  (d) anatia sahihi nyaraka –  (i) kwa jina la mtu yeyote bila ya ruhusa ya mtu huyo, liwe jina hilo ni la yule anayetia sahihi hiyo au silo;  (ii) kwa jina la mtu yeyote wa kubuniwa ambaye anadhaniwa kwamba yupo, iwe mtu wa kubuniwa huyo anadhaniwa kwamba ni wa jina sawa na aliyetia sa...

ENVIRONMENTAL MANAGEMENT ACT

MAELEZO YA KIFUPI KUHUSU SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 Sehemu ya kwanza Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ambayo inakusudia kuweka muundo wa kisheria na taasisi utakaoweka usimamizi endelevu ya mazingira katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira. Muswada huu unaainisha misingi ya usimamizi wa mazingira kama vile Kanuni ya msingi ya haja ya kuchukua tahadhari panapokuwa na wasiwasi kuwa shughuli inayotaka kufanyika itakuwa na madhara kwa mazingira; basi isifanyike hata kama hakuna ushahidi wa kisayansi. Kanuni nyingine ya msingi ni ya mchafuzi kuwajibika kulipa gharama za kusafisha uchavuzi au kurekebisha uharibifu alioufanya. Sehemu hii pia ina kanuni ya msingi juu ya ushirikishwaji wa jamii katika utayarishaji wa sera, mipango na michakato ya usimamizi na hifadhi ya mazingira Sehemu ya Pili ina misingi mikuu inayotumika katika usimamizi wa mazingira pamoja na wajibu wa kulinda mazingira. Sehemu inapendekeza vifungu vya sheria vitakavyohakikisha haki kwa kila mtu aliyepo ...