Posts

MAKOSA YA JINAI  YA  UVIVU NA UZEMBE

MAKOSA YA JINAI  YA  UZEMBE NA UVIVU Sheria yetu ya kanuni ya adhabu inatambua makosa ya uvivu na uzembe kama makosa ya jinai yanayoadhibiwa kisheria, fungu la 176 ya kanuni ya Adhabu. ü   Kucheza kamari kuwa ni kosa la jinai ü   Kufanya umalaya ü   Kufanya kitendo cha aibu mbele ya hadhara/ kufanya mapenzi mbele ya watu. ü   mtu aliyeajiriwa chini ya ajira halali inayotambulika ambaye, bila udhuru halali, anapatikana akichezacheza au kufanya mzaha wakati wa muda wa kazi, atahesabiwa kuwa ni mtu mvivu na mzembe na atapaswa kulipwa faini isiyozidi shilingi mia tano au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja. ü   mtu anayetangatanga au anayejiweka katika mahali popote pa hadhara kwa kuomba au kukusanya sadaka, kumtuma au kumhimiza mtoto kufanya hivyo; ü   mtu anayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa namna yoyote kwa njia ya kujisingizia au hadaa; ü   mtu anakayeonekana ndani au ...

MAKOSA YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE

Image
MAKOSA YA JINAI YATOKANAYO NA UZEMBE Makosa ya uzembe mbali ya kuwa makosa ya madai ambayo yaadhibiwa na sheria pia ni makosa ya jinai kulingana na sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 233. Mtu yeyote ambaye kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine yeyote:- (a) anaendesha gari lolote , baiskeli au piki piki katika barabara yoyote ya umma; au (b) anaendesha au kushiriki katika kuendesha au kufanya kazi katika meli yoyote; au (c) anafanya kitendo chochote kwa kutumia moto au kitu chochote kiwezacho kuwaka au kuacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambao inaweza kutokea kutokana na moto wowote au kitu chochote anachomiliki ambacho kinaweza kuwaka; (d) anaacha kuchukuwa tahadhari dhidi ya hatari yoyote ambayo inaweza kutokea kutokana na mnyama yoyote anayemmiliki; au (e) anatoa matibabu ya dawa au ya upasuaji kwa mtu yeyote ambaye amediriki kumtibu; au (f) anachanganya, a...
Image
JE MKE ANAWEZA KUMUIBIA MUME WAKE, AU MUME ANAWEZA KUMUIBIA AU KUIBA MALI YA MKE. Ni swali linaloulizwa na watu wengi sana wakitaka kufahamu kama mume na mke wanaweza kuibiana, kulingana na sheria yetu Kanuni Ya Adhabu (Penal Code) Kifungu cha 264 Ili kuondoa mashaka, inatangazwa hapa kuwa mume anaweza kuwa na hatia kwa kumuibia mke wake au mke kwa kumuibia mumewe. Hii inatokana na maana ya kisheria inayotolewa katika Kifungu cha 258 ya Kanuni Ya Adhabu, (1) Mtu ambaye kwa udanganyifu na bila ya dai la haki anachukua kitu chochote ambacho kina uwezo wa kuibwa, au kwa udanganyifu anabadili matumizi ya mtu yeyote tofauti na mmiliki wa jumla au maalum wa kitu chochote chenye uwezo wa kuibiwa, atakuwa anaiba kitu hicho. (2) Mtu yeyote ambaye anachukua au anabadilisha kitu chochote ambacho kina uwezo wa kuibwa, anachukuliwa kufanya hivyo kwa udanganyifu iwapo anafanya hivyo akiwa na nia yoyote kati ya hizi, hii ni kusema- ü   (a)nia ya la kumnyang’anya kabisa mmiliki wa juml...

KOSA KUSHANGILIA AU KUCHOCHEA WATU WANAOTENDA UHALIFU (SOLICITATION AND INCITEMENT)

Image
JE WAJUA KUWA KUSHANGILIA AU KUCHOCHEA AU KUSHADADIA WATU WANAPIGANA AU KUTENDA UHARIFU NI KOSA LA JINAI. Pamoja na Tanzania kuwa nchi ya amani lakini pia watu wameendelea kutenda makosa ya jinai yanayo hatarisha amani bila kujua na kuchochukuliwa hatua za kisheria kwa sababu matukio haya yanafahamika lakini hayaripotiwi. Kanuni Ya Adhabu 390. Mtu yeyote ambaye anamshawishi au anamchochea mtu mwingine kutenda kosa, atakuwa anatenda kosa bila kujali kwamba ushawishi au uchochezi huo hauna madhara.
Image
KOSA LA KUAZIMISHA NA KUAZIMISHA  VYETI Hili ni kosa la jinai ambapo anaazimisha cheti kwa mtu mwingine akiwa na lengo la kukitumia kwa manufaa Fulani, hili kosa linaadhibiwa kisheria baada ya mtuhumiwa kupatikana na hatia kuwa aliazimisha cheti chake kitumike na mtu mwingine kinyume cha sheria Kanuni ya Adhabu Kifungu cha 373, kinaeleza kama ifuatavyo ’’Mtu yeyote ambaye, akiwa yeye ndiye aliyepewa nyaraka yoyote iliyotolewa na mamlaka halali ambapo amedhibitishwa kuwa ni mwenye sifa zozote zinazotambulika na sheria kwa madhumuni yoyote, au kuwa ni mwenye ofisi yoyote, au kuwa na haki ya kufanya kazi ya taaluma yoyote, biashara, au kuwa na haki yoyote au upendeleo, au kwa kutumia cheo chochote au hadhi, anauza, anatoa au anaazima nyaraka hiyo kwa mtu mwingine kwa dhamira kwamba huyo mtu mwingine anaweza kujiwakilisha kuwa yeye ndiye mtu aliyetajwa katika nyaraka  hiyo, atakuwa anatenda kosa’’ Sheria imeenda mbali zaidi na kutambua kuwa hata aliyeazima cheti hicho anaku...

KOSA LA KUVUNJA NYUMBA KULINGANA NA SHERIA YETU

Image
KOSA LA KUVUNJA NYUMBA (HOUSEBREAKING & BULGRALY) Kosa hili la jinai linahusisha mtu kuingia na kuvunja katika jengo lolote linalotumika kama makazi ya kuishi binadamu kwa dhamira ya kutenda kosa Yafuatayo yanahusisha kosa la kuvunja nyumba Ø   (1) Mtu ambaye anavunja sehemu yeyote,, iwe nje au ndani ya jengo, au anafungua mlango uliyofungwa, anavuta, anasukuma au anainua, au kwa namna nyingine yoyote, mlango wowote, dirisha, kifungio chochote, kilango cha dari au kitu kingine, ambavyo vimekusudiwa kufunga au kuziba uwazi katika jengo hilo, au uwazi unaotoa njia ya kutoka sehemu moja ya jengo mpaka nyingine, anachukuliwa kuwa amevunja jengo hilo. Ø   (2) Mtu anachukuliwa kuingia ndani ya jengo mara tu ambapo sehemu yoyote ya mwili wake au sehemu yoyote ya chombo chochote alichokitumia kipo ndani ya jengo hilo. Ø   (3) Mtu ambaye ameingia ndani ya jengo kwa njia za kitisho au hilo itumikayo kwa haja hiyo, au kwa kushirikiana kwa hila na mtu yeyote aliyemo nd...

KOSA LA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI

Image
JE UNAJUA KUWA KUHAMISHA MIPAKA YA ARDHI KWA LENGO LA KUDANGANYA NI KOSA LA JINAI Watu wengi wamekuwa wakitenda kosa la kuhamisha mipaka kwa lengo la kudanganya na kujiongezea ukubwa wa maeneo yao wanayomiliki, lakini hili jambo limekuwa mara nyingi limechukuliwa kama kosa la madai, lakini kulingana sheria yetu ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 linatumbuliwa kuwa ni kosa la jinai. Kifungu hicho kinaeleza kama ifuatavyo. ’’ Mtu yeyote ambaye, kwa kunuwia na isivyokuwa halali na kwa nia ya kudanganya, anaondosha au anafuta kitu chochote au alama ambayo iliyowekwa kihalali kama alama ya mpaka wa ardhi yoyote atakuwa anatenda kosa  la jinai’’ ADHABU KWA ALIYEHAMISHA MIPAKA Adhabu yake kulingana na Kanuni ya Adhabu kifungu cha 329 ni Miaka mitatu endapo mtuhumiwa atakuwa amepatikana na hatia. Hivyo mnashauriwa mridhike na mipaka ya maeneo yenu ili kuepuka adhabu hii inayotolewa na sheria.
Image
KOSA LA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE Kulingana na watu kuwa wabunifu wa kutenda dhambi na kuongezeka kwa maarifa, tafiti zinaonesha ukatili wa jinsia unaongezeka na idadi ya talaka pia zinaongezeka kwa sababu ya watu kufanya kamchezo kanakojulikana kama kuruka ukuta na kusukuma tope yaani kufanya mapenzi kinyume cha maumbile. Kulingana na sheria yetu ya Kanuni Ya Adhabu (Penal Code) kifungu cha 154 kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni  kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha maisha. Mtu yeyote ambaye anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au, anamuingilia mnyama kimwili au  anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile, atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini . Lakini  Ikiwa kosa limetendwa  dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha hii ni kulingana na kanuni ya Adhabu(...

KOSA LA KUVAMIA ARDHI/ CRIMINAL TRESPASS NA ADHABU YAKE KULINGANA NA SHERIA ZETU

Image
KOSA LA KUINGIA KWA  JINAI (CRIMINAL TRESPASS)  AU UVAMIZI WA  ARDHI Kanuni ya Adhabu kifungu cha 299 kinaeleza kuwaMtu yeyote ambaye Isivyokuwa halali anaingia ndani ya mali inayomilikiwa na mwingine kwa kusudi la kutenda kosa au kumtisha, kumtukana au kumuudhi mtu yeyote mwenye kumiliki mali hiyo au ameingia kwa halali ndani ya mali hiyo na bila ruhusa halali akabaki humo kwa kusudi la kumtishia, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo au kwa kusudi la kutenda kosa. atakuwa anatenda kosa la kuingia kwa jinai ADHABU YA KUINGIA KWA JINAI Adhabu yake ni kifungo cha miezi mitatu hii ni kwa mtu aliingia isivyohalali ndani ya mali inayomilikiwa  Ikiwa mtu ameingia ndani ya mali ilivyo halali kwa ruhusa lakini bila ruhusa au idhini akaendelea kubaki ndani ya eneo kwa lengo la kumtisha, kumtukana au kumuudhi mtu anayemiliki mali hiyo adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja NAMNA NYINGINE YA KUPATA FIDIA KWA ARDHI ILIYOVAMIWA Zingatia kuwa unaweza kufan...

KOSA LA KUGHUSHI NA ADHABU YAKE

Image
KOSA LA KUGHUSHI VYARAKA MBALIMBALI Kanuni ya Adhabu kifungu cha 333 kinaeleza nini maana ya kughushi ikiwa ni ni kutengeneza nyaraka ya uwongo kwa nia ya kudanganya au kuhadaa. Kanuni ya Adhabu kifungu cha 335 kinaeleza kuwa. Mtu yeyote anayetengeneza nyaraka ya uwongo ambaye–  (a) anafanya nyaraka ambayo ni ya uwongo au ambayo ana sababu ya kuamini kuwa si ya kweli;  (b) anabadili nyaraka bila ya mamlaka kwa namna ambayo iwapo kubadili huko kungekuwa na mamlaka kungebadili matokeo ya nyaraka hiyo;  (c) anaingiza katika nyaraka hiyo bila ya mamlaka , wakati nyaraka hiyo inaandikwa, jambo ambalo kama lingeruhusiwa lingebadilisha matokeo ya nyaraka hiyo;  (d) anatia sahihi nyaraka –  (i) kwa jina la mtu yeyote bila ya ruhusa ya mtu huyo, liwe jina hilo ni la yule anayetia sahihi hiyo au silo;  (ii) kwa jina la mtu yeyote wa kubuniwa ambaye anadhaniwa kwamba yupo, iwe mtu wa kubuniwa huyo anadhaniwa kwamba ni wa jina sawa na aliyetia sa...

ENVIRONMENTAL MANAGEMENT ACT

MAELEZO YA KIFUPI KUHUSU SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 Sehemu ya kwanza Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ambayo inakusudia kuweka muundo wa kisheria na taasisi utakaoweka usimamizi endelevu ya mazingira katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira. Muswada huu unaainisha misingi ya usimamizi wa mazingira kama vile Kanuni ya msingi ya haja ya kuchukua tahadhari panapokuwa na wasiwasi kuwa shughuli inayotaka kufanyika itakuwa na madhara kwa mazingira; basi isifanyike hata kama hakuna ushahidi wa kisayansi. Kanuni nyingine ya msingi ni ya mchafuzi kuwajibika kulipa gharama za kusafisha uchavuzi au kurekebisha uharibifu alioufanya. Sehemu hii pia ina kanuni ya msingi juu ya ushirikishwaji wa jamii katika utayarishaji wa sera, mipango na michakato ya usimamizi na hifadhi ya mazingira Sehemu ya Pili ina misingi mikuu inayotumika katika usimamizi wa mazingira pamoja na wajibu wa kulinda mazingira. Sehemu inapendekeza vifungu vya sheria vitakavyohakikisha haki kwa kila mtu aliyepo ...

Fidia kwa ardhi iliyotwaliwa kwa manufaa ya umma kulingana Sheria za Ardhi

Image
FIDIA YA ARDHI NI NINI. Fidia ya ardhi ni stahili ambayo mwenye ardhi mmiliki anatakiwa kupata pale ambapo ardhi yake inatwaliwa/inachukuliwa na serikali kwa matumizi maalum ya serikali/umma. JE UNAWEZA KUIKATALIA SERIKALI ARDHI YAKO ISICHUKULIWE ? . Serikali inapotaka kumhamisha mwananchi na kuchukua ardhi yake kupisha mradi wa umma kisheria mwananchi hana uwezo wa kukataa. Hii ni kwasababu ardhi yote ni mali ya umma ambayo mdhamini wake mkuu ni serikali kupitia mamlaka ya rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa ardhi ni mali ya umma inayodhaminiwa na serikali/rais. Kwa hiyo mwananchi hawezi kuikatalia serikali kuchukua mali hiyo isipokuwa kisheria ni kuwa anayehamishwa apewe fidia.  Hata ukiamua kwenda mahakamani kupinga kutwaliwa ardhi hautapinga kuwa serikali isichukue ardhi yako kabisa, isipokuwa utapinga kuhusu fidia, labda fidia ndogo au utaratibu mbovu uliotumika ku...

FAHAMU MISINGI YA SHERIA YA ARDHI YA TANZANIA

Image
FAHAMU MISNGI YA SHERIA YA ARDHI YA TANZANIA Ifuatayo ni misingi halisi ya ardhi kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo wa ardhi wa kitaifa (sera) na kutafsiriwa na sheria mbalimbali za nchi: i. Ardhi yote ni mali ya umma na imekabidhiwa kwaRaisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya watanzania wote; ii. Kulinda haki zote za miliki za ardhi zilizopo, yaani miliki ya ardhi ya kimila na ile ya kiserikali; iii. Kugawa ardhi kwa haki na kwa raia wote wa Tanzania; iv. Kudhibiti kiasi ambacho mtu mmoja au taasisi yaweza kumiliki na kutumia kwa mahitaji yake bila kuwaathiri Watanzania au wanajamii wengine; v. Kuwezesha utumiaji endelevu wa ardhi katika shughuli za kiuzalishaji kwa manufaa ya wote; vi. Kuhakikisha kwamba maslahi yeyote katika ardhi yana thamani na yanalindwa katika muda wowote wakati wa mapatano yanayoweza kuathiri thamani ya mmiliki; vii. Kulipa fidia kamili na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki ya ardhi yake inafutwa, inabadi...

Express and Implied Rights and Duties of Employee Under Employment and Labour Relation Act

Image
Express Rights and Duties  The express rights and duties in a contract of employment are provided by the parties expressly in the contract of employment. Worth remembering is the fact that express rights and duties may either be written or oral depending on the type of the contract. Matters such as leave, salary, overtime, hours of work, job description, job title, holidays, sick pay, pension, notice, confidentiality, restraints, disciplinary and grievance procedure, are covered by the express terms. In most cases these contents are provided in standard form to the employees with little room for negotiation.  However, the various sources of express terms could include a formal contract, a letter of appointment, a statutory statement of the main terms and conditions, oral statements made prior to the contract and even the job advertisement.  Note:  1. It should be noted that express statements become part of the contract only if they were made prior t...